Ndugu ,
Kwanza kabisa napenda nitoe shukrani kwako kwa kutembelea tovuti hii ya Halmashauri ya wilaya ya Meatu,
Ikiwa ni jitihada za Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa awamu ya tano ya Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli
Pili, Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa
1) Bila ya kuathiri sheria ya nchi, na kutafuta,kupata na kueneza au kusambaza habari na mawazokupitia chombo cha habari chochote bila ya kujali mipaka ya taifa pia anayohakina uhuru wa kutoingiliwa na mawasiliano
2) Kila raia ana haki ya kupashwahabari wakati wote kuhusu matukio mbalimbali ya nchini na duniani kote yenyeumuhimu kwa maisha na shughuli za wananchi , pia kwa masuala yenye umuhimu kwajamii.
3) Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu maswala muhimu ya jamii
Kwa kuzingatia mambo niliyoyataja hapo juu,
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ilizindua tovuti hii katikati ya mwezi Februari, 2017 na itakuwa daima kuwa "kazi inayoendelea". Tutaendelea kuongeza yaliyo muhimu kwenye tovuti yetu ili kuifanya kuwa kituo cha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa umma. Tafadhali tujulishe nini ungependa kuwak inapatikana kwenye tovuti yetu ili kukusaidia kufaidika kwa kutumia anwani zilizopo katika sehemu ya wasiliana nasi.
Mwisho tunatarajia kwamba utarudi mara kwa mara ili kufuatilia jitihada zetu za kutoa huduma kwa raia wa Meatu na umma kwa ujumla.
Karibu sana
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.