Wilaya ya Meatu ni wilaya mojawapo ya wilaya tano za Mkoa wa Simiyu, Tanzania Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 299,619.
Makao makuu ya wilaya yapo Mwanhunzi. Eneo lake ni kilomita za mraba 8,835.
Hali ya Hewa
Eneo la Meatu ni nusu yabisi yaani haipokei mvua nyingi. Kiwango cha mvua kinapungua kutoka kaskazini kuelekea upande wa kusini ambako ni milimita 400 za pekee zinazonyesha kwa mwaka ilhali sehemu za kaskazini zapokea milimita 900. Kiwango cha mvua huweza kuwa tofauti kila mwaka ambayo ni tatizo kwa ajili ya wakulima.
Uchumi
Uchumi kwa jumla ni wa kilimo na ufugaji. Mazao ya chakula ni hasa mahindi na mtama lakini kilimo cha mahindi huwa na matatizo ya mara kwa mara kutokana na mabaduiliko ya kiwango cha mvua. Kwa hiyo kila baada ya miaka mitano kuna uhaba wa chakula. Wanawake hulima mahali pengi viazi vitamu karibu na mito ya muda mahali ambako ipo.
Udongo hasa upande wa kusini una kiwango kikubwa mno cha magadi na hivyo hufai kwa kilimo cha muhogo ambalo ni zao linalovumulia ukame.
Ufugaji ni muhimu katika wilaya na wastani ya ng'ombe ni 12-13 kila kaya lakini kwa tofauti kati ya ng'ombe 0 na 2,00 kwa kaya.
Zao la biashara muhimu zaidi ni pamba. Watu wameanza kujenga vinu vya kuchambulia pamba kwa hiyo soko la pamba limeboreshwa hata kama mwendo huu unaweza kuleta matatizo ya chakula. Meatu ni eneo lenye pamba nyingi katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga.
Utalii ni tawi la uchumi lililoanza kuchipuka kutokana na nafasi ya kuwinda.
Uchimbaji wa vito pamoja na chumvi umeanza hapa na pale kwa kutumia mbinu za kienyeji.
Mipaka
Meatu imepakana na Wilaya ya Bariadi upande wa kaskazini, Wilaya za Karatu, Ngorongoro na Mbulu upande wa mashariki, Mkoa wa Singida na Maswa upande wa magharibi na Sinyanga upande wa kusini
Maeneo ya Kuhifadhiwa
Karibu nusu ya wilaya ni maeneo yaliyohifadhiwa ambayo ni
Maeneo mengine ya 4,582 km2 ni ardhi ya kilimo na ufugaji.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.