Na Benton Nollo, Mwanhuzi.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura amewapongeza Wataalam wa Halamashauri ya Wilaya hiyo kwa maandalizi mazuri ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa kuzingatia vigezo na vipaumbele stahiki.
Ngatumbura ametoa pongezi hizo wakati wa kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022, nusu mwaka wa fedha 2022/2023 na mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambacho kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu tarehe 27 Januari 2023.
"Ninawapongeza sana Wataalam na Waheshimiwa Madiwani kwa maandalizi mazuri ya Bajeti ya Halmashauri kwani imezingatia vipaumbele vya kitaifa na vya wilaya yetu...tusubiri mchakato wake ukamilike ili kwa pamoja tusimamie utekelezaji wake." Amesema Ngatumbura.
Baraza hilo limeridhia na kupitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo imekadiria kukusanya na kutumia shilingi bilioni 39.97.
Kati ya fedha hizi Mapato ya Ndani ni shilingi bilioni 3.22 na kufanya ongezeko la asilimia 10 ukilinganisha na Bajeti ya mwaka 2022/2023 ambapo Bajeti ya Halmashauri ilikuwa shilingi bilioni 38.3.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.