Na Linus R. James
Wazalishai wa chumvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wamewezeshwa mashine ya kisasa ya kuchanganya chumvi pamoja na madini joto. Hayo yamebainishwa mapema leo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Meatu ambapo ofisi ya mkurugenzi imepokea mashine pamoja na jenerata la kuiendesha vyenye takribani kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 26 kutoka katika shirika la NUTRION INTERNATIONATIONAL Kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na lishe walioambatana na uongozi wa mkoa wa Simiyu.
Akizungumza kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa wa Simiyu Ndg. Chacha Magigealisema kwamba maagizo ya katibu tawala ofisi ya mkurugenzi ihakikishe inawashirikisha wazalishaji wa chumvi.
“ Hii mashine ni kwa ajili ya wazalishai, kwa hiyo muhakikishe mnawashirikisha. Mfanye nao kazi pamoja na muhakikishe mnawaeleza faida za hii mashine.”
Pia alisisitiza kuwa wanahitaji kuwa wanapata taarifa ya mashine hii ili kuweza kujua kama kuna mahitaji zaidi ya mashine na ni kwa kiasi gani.
Mbali na mashine hiyo iliyotolewa Afisa Lishe wa Wilaya ya Meatu, Bi Zuwena Abbas alisema tayari kuna mashine nyingine ambayo iko katika hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kupima kiwango cha madini joto lengo likiwa ni kuhakikisha chumvi inayosafirishwa au kutumiwa katika wilaya ya Meatu inakua na kiwango cha madini joto kinachotakiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Bi Mwanaisham Nassor aliwashukuru wadau na uongozi wa mkoa kwa kutoa msaada wa mashine hiyo na kuwahahidi kuwa uongozi wa Meatu utweka mpango kazi ikiwa ni pamoja na uhamasishaji na mahali na lini mashine itafungwa.
“Uongozi wa Halmashauri utateua wajumbe kwa ajili ya kushirikiana na wananchi ili kubaini sehemu sahihi ya kufunga mashine na kasha tutafunga mashine ili ianze kazi mara moja kabla au ifikapo tarehe 15 mwezi Septemba”. Alisema Bi Mwanaisham.
Aidha uongozi wa Wilaya ya Meatu uliomba uongozi wa mkoa kwamba mara ikifika hatua ya kufunga mashine watamuomba mtaalam kwa ajili ya kuja kusaidia ufungaji pamoja na mafunzo ya matumizi ya mashine hiyo
Mashine hii ni jitihada za kuondoa athari za madini joto katika mkoa wa Simiyu hususani mkoa wa simiyu ambapo takwimu mbali mbali zinaonesha kiwango cha kutumia chumvi ya madini joto bado kipo chini licha ya kuwepo kwa sharia inayokataza matumizi ya chumvi isiyo na madinijoto.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.