Na Linus R James - MEATU DC
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Ndg. Fabian Manoza mapema leo alipofanya ziara katika shule ya Sekondari Mwanjoro na kuzungumza na wazazi, walimiu, wanafunzi na watumishi wa kata ya Mwanjoro.
Katika kikao hicho kilichokua na lengo la kupanga mkakati wa namna ya kupata utatuzi wa changamoto ya upungufu wa viti na meza(madawati) kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mwanjoro mkurugenz huyo licha ya kuahidi kutoa mifuko 100 ya saruji, madawati 10 pamoja na kutoa motisha kwa mwanafunzi yoyote atakayepata daraja la kwanza(div one) pia ameguswa sana na kupongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na uongozi wa kata hiyo kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri pamoja na wanakijiji katika kuinua elimu ikiwa ni pamoja najitihada za kujenga bweni la wanafunzi wa kike ambalo lipohatua ya lenta ya pili na ujenzi unaendelea.
Akizungumza na wanafunzi na walimu baada ya kikao cha wazazi Mkurugenzi huyo ametoa ahadi ya shilingi elfu hamsini kwa mwanafunzi yeyote atakayetoa taarifa kwa mtu yeyote atakayejihusisha kimapenzi na mwanafunzi.
Licha ya kutoa ahadi hiyo Mkurugenzi huyo ameoneshwa kukerwa na na matokeo yasiyoridhishwa ivyo kuhahidi kumshughulikia mtu yeyote atakayejihusisha kimapenzi ikiwa ni pamoja na wanafunzi, walimu au wanakijiji.
"Lakini huku bado tuko nyuma, matokeo ya kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo bado hatufanyi vizuri hata kimkoa, mwaka huu kidogo tumeinuka, nawashukuru sana walimu na wazazi ambao sasa wameinuka na viongozi wetu kwa ushirikiano tunaoupata, lakini kiukweli bado tunahitaji jitihada za ukweli kuhakikisha wanafunzi wetu wanafanya vizuri" Alisema Ndg. Manoza
Katika kikao hicho chenye lengo la kupata madarasa, wanakijiji wa Kata ya Mwanjoro na Mbushi wameahidi kutengeneza madawati yanayopungua na kuyakamirisha ifikapo tarehe 25 mwezi wa tatu mwaka huu.
Akiwasalimia wazazi Mkurugenzi huyo alitaja jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania chini ya Dk. John Pombe Magufuri katika elimu na kuwaonesha ni nama gani wazazi hao wanatakiwa waoneshe kumpongeza kwa vitendo alijaribu kutoa mfano wa fedha za elimu bure zinazokuja katika shule hiyo.
"Nilikua natoa mfano wa Rais wetu wa awamu ya tano, Mh Dk John Pombe Magufuli, hela inayotoka serikalini kuja hapa mwezi mmoja tu tumepokea shilingi 531,453 mwezi mmoja tu, sasa hii ukizidisha mara kumi na mbili, ukazidisha kwa shule zote Tanzania, ni Matrilioni ya hela Mh Rais anatoa kuwafidia watoto wetu wasome, sasa tunahitaji na sisi kumpongeza Mh Rais wetu kwa vitendo kwa yale ambayo yapo chini yetu sisi wazazi tuyafanye".
Katika kikao hicho wanakijiji hao waliweza kumchagua Ndg Ibrahim kuwa mwenyekiti, wazazi wawili(mmoja kutoka kila kata) kuwa makatibu wa kusimamia zoezi hilo amabapo zoezi hilo kila dawati litakua na thamani ya shilingi elfu 40 ambapo fedha zitakusanywa na madawati yatatengenezewa mjini Mwanhuzi. Aidha Mkurugenzi huyo ameahidi ofisi yake kutoa gari ambalo litayasafirisha madawati hayo pindi yatakapokamilika kutoka Mjini Mwanhuzi mpaka shule ya Sekondari Mwanjoro.
Pia mkurugenzi ametoa ahadi ya ofisi ya Mkurugenzi mtendaji kumsomesha kuanzia kidato cha tano hadi cha sita popote pale atakapochaguliwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwanjoro aliyefanya vizuri kimasomo katika matokeo ya kidato cha nne ambapo amepata daraja la kwanza
Kikao hicho kiliudhuriwa na wakuu wa idara mbali mbali za Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,Mh Diwani wa viti maalumu pamoja na Mh Diwani wa kata ya mwanjoro na wataalamu mbali mbali ngazi ya Kata ya Mwanjoro na Mbushi.
Mwisho.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.