Na Linus R. James (MEATU DC)
Hayo yamesisitizwa jana na katibu mkuu wa Mifugo katika Wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi Prof. Ole Sante Ole Gabriel katika kikao kazi chake kati ya uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu pamoja na wafugaji wa Wilaya ya Meatu.
“Tunatamani fikra za wafugaji wa Meatu na kote nchini, zibadilike na ziweze kutambua umuhimu wa sheria, taratibu na kanuni, Niwaombe wafugaji wa Meatu, simiyu, kanda ya ziwa na Tanzania nzima popote walipo watambue kwamba Wizara ya mifugo ya uvuvi itapenda wafugaji wake wafuate kanuni, taratibu na miongozo” Alisema Ptof Ole Sante
Licha ya kusisitiza umuhimu wa kufuata sharia za nchi Katibu mkuu huyo alisisitiza mambo makuu manne aliyokuja kuyasisitiza kubwa likiwa ni umuhimu wa kufata sharia na taratibu za nchi, mengine yalikua ni masuala ya uhamirishaji, Ufugaji wa kisasa uunganike na uchumi wa viwanda
Pamoja na Wakulima wkutobweteka na mifugo wajali uchumi wao ikiwa ni kuvaa vizuri na kuwa na maisha mazuri.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Ndg. Fabian Manoza mbali na kutoa shukrani alibahinisha jitihada na mikakati ambayo Halmashauri ya wilaya ya Meatu inafanya ili kuboresha kiwanda cha maziwa ambapo tayari kupitia Wizara ya Kilimo tayari mashamba darasa ya malisho yamepandwa katika shamba la Halmashauri ya Wilaya ya Meatu na katika kata ya Lubiga ikiwa ni jitihada za kuwa na uhakikika wa malisho.
Pia alikielezea kikao kuwa tayari halmashauri ya Wilaya imeanza kugawa mbegu za uhamirishaji na baadhi ya wafugaji walipo katika kikao tayari wameshaanza kutekeleza suala la uhamirishaji.
Viongozi mbali mbali wa Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dr. Joseph Chilongani, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (W) Meatu Ndg. Juma Mwiburi waliweza kumshukuru Katibu mkuu kwani safari yake imeonesha na kuboresha hali ya mawasiliano na ukaribu baina ya uongozi wa Wilaya ya Meatu na wafugaji ambao ni wananchi wanaowatumikia.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi mbele ya kikao diwani wa kata ya Mwasengera Mh Saakumi aliwasisitiza wafugaji wenzake suala la kuzingatia taratibu na sheria ziheshimiwe
“Tatizo tulilokua tunaliona ni kati ya wahifadhi wanaotekeleza sharia na sisi, Upo ubabe uliokuwa unazidi sana, vitu ambao tumebaini kwenye kikao chetu ni sisi viongozi na wahifadhi, tatizo tulilo nalo sisi ni pale tunapokamatwa, katika kikao chetu cha ndani tumefikia muafaka kuwa sisi ni wamoja kati ya wahifadhi na viongozi” Alisema Mh Saakumi
Katika kikao hicho Mwenyekiti wa CCM wilaya alipewa jukumu la kukutana na wafugaji kwenye maeneo yao ya ufugaji ndani ya wiki mbili kuhakikisha changamoto na kero zote zinajadiliwa na kutatuliwa haraka ili Wilaya ya Meatu iwe na ufugaji wenye tija.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.