Na Benton Nollo, Mwanhuzi
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura amewataka Wafanyabiashara na Wananchi wote wilayani humo kuwa na utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya biashara na ya makazi.
Ngatumbura ameyasema hayo mapema leo tarehe 06 Desemba 2022 mara baada ya kufanya zoezi maalum la usafi katika Soko Kuu la Mwanhuzi na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Mwanhuzi mjini Meatu.
Mkuu huyo wa Wilaya amewaongoza Watumishi wa Umma, Wananchi pamoja na Wafanyabiashara kufanyas usafi katika maeneo hayo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ambapo kilele chake ni tarehe 9 Desemba, 2022.
“Ndugu wananchi pamoja na wafanyabiashara wote tuweni na utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yetu na tusisubiri kuhamasishwa kwani jukumu la usafi ni la kila mmoja wetu.” Amesema Ngatumbura na kuongeza;
“Mfano leo tumefika hapa stendi saa 01:00 asubuhi na kuanza usafi na kisha katika eneo lote linalozunguka soko, lakini inashangaza pamoja na matangazo yaliyotolewa tangu jana (tarehe 05 Desemba 2022) wafanyabiashara hawajitokezi na badala yake wapo waliofunga kabisa na kutoonekana…hao tutashughulika nao…wale mliojitokeza nachukua fursa hii kuwapongezeni sana na huu uwe ndiyo utamaduni wenu.”
Aidha, baada ya usafi Mkuu wa Wilaya huyo pamoja na viongozi wengine kwa pamoja wameshiriki zoezi la Upandaji miti katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu ambapo katika eneo hilo imepandwa miti 100.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Dkt. Frank Mganga amewashukuru watumishi, wafanyabiashara pamoja na wananchi waliojitokeza kushiriki zoezi la usafi ikiwa ni wiki ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania tarehe 09 Desemba 2022.
Dkt. Mganga amewakumbusha Wananchi kuwa tarehe 09 Desemba, 2022 kutakuwa na Mdahalo/Kongamano la kujadili maendeleo endelevu ambayo Wilaya ya Meatu imefikia katika kipindi cha miaka 61 ya Uhuru.
Amesema kabla ya kuanza kwa mdahalo huo ambao utafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, kutakuwa na maandamano yatakayoanzia Kituo Kikuu cha Mabasi cha Mwanhuzi mjini Meatu na kisha kuelekea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri kupitia Hospitali ya Wilaya ambapo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha kwa kuwa utahudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na Wazee Maarufu.
Kauli mbiu katika madhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ni "AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU"
Matukio Katika Picha Wakati wa Zoezi la Usafi na Upandaji Miti:
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura (aliyevaa kilemba chekundu) pamoja na viongozi mbalimbali wilayani humo wakishiriki zoezi la kufanya usafi na Wafanyabiashara wa Soko la Mwanhuzi na Kituo Kikuu cha Mabasi Mwanhuzi Meatu mjini tarehe 06 Desemba 2022, ikiwa ni kusherehekea wiki ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ambapo kilele chake ni tarehe 09 Desemba 2022.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Dkt. Frank Mganga (aliyevaa shati la bluu) pamoja na viongozi mbalimbali wilayani humo wakishiriki zoezi la kufanya usafi na Wafanyabiashara wa Soko la Mwanhuzi na Kituo Kikuu cha Mabasi Mwanhuzi Meatu mjini tarehe 06 Desemba 2022, ikiwa ni kusherehekea wiki ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ambapo kilele chake ni tarehe 09 Desemba 2022.
Viongozi, Watumishi, Wafanyabiashara pamoja na Wananchi wakishiriki zoezi la kufanya usafi katika Soko la Mwanhuzi na Kituo Kikuu cha Mabasi Mwanhuzi Meatu mjini tarehe 06 Desemba 2022, ikiwa ni kusherehekea wiki ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ambapo kilele chake ni tarehe 09 Desemba 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura (aliyevaa kilemba chekundu) akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu tarehe 06 Desemba 2022, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea wiki ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ambapo kilele chake ni tarehe 09 Desemba 2022 ambapo katika zoezi hilo miti 100 ilipandwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Dkt. Frank Mganga akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu tarehe 06 Desemba 2022, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea wiki ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ambapo kilele chake ni tarehe 09 Desemba 2022 ambapo katika zoezi hilo miti 100 ilipandwa.
Viongozi, Watumishi na Wananchi wakishiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu tarehe 06 Desemba 2022, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea wiki ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ambapo kilele chake ni tarehe 09 Desemba 2022 ambapo katika zoezi hilo miti 100 ilipandwa.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.