Anaandika Linus R. James
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Meatu Bi Fauzia Hamidu Ngatumbura katika hafla fupi ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Meatu Dr. Joseph E. Chilongani.
“Nianze na taasisi za umma zote zilizopo ndani ya Meatu, wote tunatekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi basi tutumie uwezo wetu wote kutekeleza kila mtu kwa wakati wake, kwa nafasi yake, kwa uwezo wake ambao Mungu amemtunuku na kwa ushirikiano mkubwa, ni vema tukapeana taarifa mara kwa mara kwa sababu mapungufu tunayo ili tuweze kurekebishana huku tukiendelea na safari”. Alisema Mh. Ngatumbura wakati akiwasalimu wananchi baada ya ukaribisho
Mh Ngatumbura amevihimiza pia vyama vya wafanyakazi wawaelimishe watumishi (wanachama wao) kwa kuwaelimisha kuhusu miongozo na taratibu za utumishi wa umma ili kusudi watumishi wafurahie utumishi wao na hatimaye utendaji kazi wa watumishi uboreke zaidi.
Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Meatu Bw. Fabian Manoza Said akitoa salaam na kutambulisha watendaji wa halmashauri kutoka makao makuu mpaka ngazi ya vijiji aliyataja mafanikio ambayo yamefikiwa katika uongozi wa Dr. Chilongani ikiwa ni pamoja na kupanda kwa kiwango cha ufaulu wa elimu kuanzia msingi mpaka sekondari pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa kilimo cha zao la pamba katika wilaya ya Meatu.
Hata ivyo Mkurugenzi huyo wa wilaya ya Meatu amesisitiza kuwa vipaumbele vilivyopo katika wilaya ya Meatu ni kuhakikisha wilaya, inaboresha miundombinu hususani, elimu na vituo vya kutolea huduma za afya.
“Kwenye mapambano haya mda mwingine unakuta mnasuguana, lakini mnasuguana kwa mazuri, kwenye elimu kidato cha nne kuanzia 2016 tulikua tunapandisha ufaulu kuanzia asilimia 69, mwaka unaofuata 78%, mwaka unaofuata72%, mwaka unaofuata87%, na matokeo yaliyopita asilimia 92”. Alisema Manoza ambapo alisisitiza kuwa ufaulu pia umekua ukipanda sana pia katika upande wa elimu msingi.
Kwa upande wa wananchi, Manoza amesema kipaumbele cha wilaya ni kuhakikisha uzalishaji wa zao la pamba unaongezeka kwa ekari kutoka kilo 200 kwenda mpaka kilo 600.
Naye aliyekuwa mkuu wa wilaya Dr. Chilongani akitoa salam na kuwaaaga wananchi pamoja watumishi waliodhuria hafla hiyo hakusita kuyataja mafanikio yaliyofikiwa na kumtakia kila lakheri Mkuu wa Wiaya ya Meatu.
“Mengi yameelezwa na mkurugenzi akifafanua mafanikio ambayo tumeyapata pamoja kama timu ya wana Meatu, kwa kweli tumejitahidi sana hasa kwa upande wa elimu, timu nzima ya wana Meatu tuliweza kuhakikisha tunalifanya vizuri na nina Imani zile asilimia zilizobaki kufikia asilimia 100 mtazitekeleza chini ya usimamizi wa Mh . Fauzia” Alisema Dr . Chilongani.
Hafla hii ya Kumuaga Chilongani na Kumkaribisha Bi Ngatumbura imefanyika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Meatu ambapo makabidhiano ya ofisi pamoja na taasisi zilizoko ndani ya wilaya ya Meatu yamefanyika na kisha kufuatiwa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu ambapo watumishi mbalimbali kutoka idara za afya, utumishi na afya wamepewa zawadi pamoja na kutunukiwa vyeti kutokana na utendaji kazi.
Bi. Faudhia Hamadi Ngatumbula anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu wa kumi na moja (11) toka wilaya ianzishwe baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan Tarehe 19 Juni 2021.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.