Mkoa wa Simiyu unatarajia kufanya majaribio ya kufundisha wanafunzi kwa kutumia mtandao kupitia programu itakayotengenezwa na watalaam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu Mkoani humo yaliyofanyika kimkoa mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, chini ya Kauli Mbiu “TUWEKEZE KATIKA ELIMU KWA USTAWI WA JAMII YENYE UTAALAMU WA SAYANSI NA VIWANDA KUELEKEA UCHUMI WA KATI TANZANIA”“Tunataka tufanye majaribio, tuanze kwa kuunganisha shule zetu za mjini wataalamu wetu wa ICT (TEHAMA) watengeneze programu,baadhi ya madarasa kama darasa la saba tuanze kufundisha kwa kutumia mtandao” amesema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho ya wiki ya elimu wamesema iwapo teknolojia hiyo itafanikiwa kutumika itawasaidia katika masomo yenye upungufu wa walimu hususani wa sayansi, ambapo wameiomba Serikali kuendelea kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa na vifaa vya maabara ili kuwawezesha kujifunza vema masomo hayo kwa nadharia na vitendo.Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Julius Nestory amesema maadhimisho ya wiki ya Elimu yaliyoanza Mei 24 ni moja ya tathmini ya malengo yaliyowekwa Mei 2016 na miongoni mwa mafanikio ya malengo hayo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 180 chakula cha mchana kutolewa katika shule za kutwa lililotekelewa kwa asilimia 43.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka amesema Serikali imepanga kupitia Watalaam hao wa TEHAMA pia kwa kutumia teknolojia nyepesi, itengenezwe programu itakayosaidia kutoa taarifa za uwepo wa watumishi mahala pa kazi. Soma zaidi.....
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.