Anaandika Linus R. James ,Meatu
Hayo yamebainishwa mapema leo katika kikao kazi na mafunzo katika vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Meatu
Mafunzo hayo yalioendeshwa na idara ya maendeleao ya jamii yalilkua na lengo la kutoa njia thabiti za kuviwezesha vikundi kusimamia fedha vizuri ili zilete tija na hatimaye vikundi viweze kunufaika na mikopo hiyo na kisha kufanya marejesho ya pesa.
Akimkariobisha mkurugenzi mtendaji, Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Bi Mwanaisham Nassor amesema tayari halmashauri ya wilaya imetoa Tsh 117,467,622 sawa na asilimia 95.
“Kwa mwezi Julai mpaka sasa, halmashauri imetoa Tsh. 117,676,622 sawa na asilimia 95 ya makusanyo yetu ya ndani, kwa leo vikundi vilivyopo mbele yako mkurugenzi tunaenda kutoa Tsh 85,277,00 kamili”. Alisema Bi Mwanaisham.
Bi mwanaisham aliendelea kusistiza kwamba katika mgao huo wa milioni 85, jumla yaTsh 77,777,000 zimetolewa katika vikundi 18 vya wanawake na Tshs million 10.5 katika vikundi vitatu vya vijana na milioni mbili katika kikundi cha watu wenye ulemavu.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Ndg.Msoleni Juma Dakawa akizungumza na wanaufaika wa mikopo hio alihimiza kufanya ujasiliamali wenye uwekezaji mkubwa na wenye kuleta tija ukiwa na lengo la kuongeza kipato na kutengeneza ajira kwa wananchi ama wanufaika wengi..
“Kama tukiwapa milioni 5 mkarejesha ndani ya mda mfupi (miezi mitano, sita) milioni 5 leteni maombi ya milioni tano nyingine tuwape milioni 10 lakini tunashauri mfanye biashara iliyo kubwa ambayo mwisho wa siku italeta faida kwa haraka miongoni mwenu” Alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Akitoa salam kutoka upande wa afya Kaimu mganga Mkuu wa Wilaya Dr.Frank Mganga aliwasisitiza wamnavikundi kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari dhibi ya virusi vya UVIKO 19 na kuwasisitiza watu wachanje kwa hiari.
“ Chanjo inakuepusha usipate gharama hizi hela mnazopewa zina marejesho, kwa mfano kama watu watatu wakiugua kwenye kikundi mnafanyeje, sasa chanjo inapatikana na chanjo inapatikana hapa hapa ukumbini kwa hiyo nawashauri mpate chanjo”. Alisisitiza Daktari.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum Meatu Mh. Minza Simon Mjika aliwasistiza wana vikundi kuangalia faida na hasara katika biashara wanazozifanya kwa kuweka kumbukumbu na kuangalia mapato na matumizi.
“ Jifunze kwenda kwa mahesabu, unataka kuchoma chapati chukua mzani pima weka kwenye chombo angalia unata chapati ngapi mwisho wa siku ujue faida. Usipike wakati unapika mwisho wa siku utaungua moto tuu, jifunze kufanya kitu kwa malengo”. Alisema Mh Mbunge.
Hafla na mafunzo hayo yameudhuriwa na Mbunge wa viti maalum Jimbo la Meatu Pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu ambapo baada ya mafunzo na nasaha, hundi ya mfano ilitolewa kwa wanakikundi.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.