Na Linus R. James Meatu DC
Hayo yamebainishwa katika mkutano uliofanyika jana katika ukumbi wa halmashauri ya Meatu baina ya Naibu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera, kazi, vijana na ajira ya Masuala ya watu wenye ulemavu Mh Stella Ikupa na viongozi mbali mbali halmashauri , serikali na chama Tawala wa Mkoa wa Simiyu pamoja na watu wenye ulemavu Meatu.
Akimkaribisha Naibu waziri, mbunge wa viti maalum(CCM) wilaya ya Meatu Mh Leah Komanya alimkumbusha naibu waziri huyo ombi la vifaa saidizi vya walemavu ikiwa ni pamoja na viungo na baiskeli.
“Najua mengi yanafanywa katika ofisi ya Waziri Mkuu upande wa walemavu tumekua tukiona sehemu zingine walemavu wanapewa vifaa vya kuwawezesha vikiwemo viungo, nimekua nikuletea sana kabla hujawa hata waziri ombi la ‘wheel chair’ za walemavu na picha nikuonesha walemavu walivyo naomba sana unisaidie katika Wilaya hii nimefurahi upo na walemavu wapo na wanamuona Mbunge yupo ambaye anawasemea ninakuomba useme chochote utakapopata nafasi ya kuongea nao”. Alisema Mbunge huyo.
Licha ya Naibu waziri huyo Kuupongeza uongozi wa Wilaya hususani kwa jitihada mbali mbali hasa kuwaweza walemavu kushiriki mambo mbali mbali ndani na nje ya Wilaya na kuwapatia mkopo usio na riba, yapo mambo ambayo kikao hicho kiliona ni muhimu kuyatilia mkazo ili kuhakikisha watu wenye ulemavu mbali mbali wanaweza kufanya shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha pia kundi la walemavu linashiriki katika mradi wa kitalu nyumba unaendelea utekelezwa wilayani .
Naye Naibu waziri aliahidi kuwa kwakua kuna vifaa vipo karibuni kuja wizarani ivyo anawaahidi kuwa vitakapofika katika atajitahidi kuhakikisha na Wilaya ya Meatu inapata vifaa katika mgao unaokuja pia aliweza kusisitiza kuhakikisha makundi ya watu wenye ulemavu wanajiunga katika mfuko wa CHF iliyoboreshwa.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya alibainisha mambo makubwa ya mda mrefu ambayo ofisi imejipanga ambayo ni pamoja na Halmashauri kuwa na mpango wa kuwajengea ofisi maalum kwa ajili ya kuratibu mambo yao, kuhakikisha mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanapatikana kwa wakati na na kuhakikisha makusanyo yanakusanywa kwa ufanisi ili fedha za kuwakopesha watu wenye ulemavu zinapatikana kwa wakatii.
Akimkaribisha Mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ndg. Mh Festo Kiswaga mbaye ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi aliweza kutaja vipaumbele vya mkoa ambavyo ni Elimu na Kilimo na kwakua mkoa upo kwenye mchakato wa kila kijiji kuwa na kiwanda alisema fursa ya kilimo hususani kitalu nyumba ni nyenzo muhimu kufikia jitihada za mkoa.
”Mh RC ametoa vipaumbele viwili cha kwanza ni Elimu cha pili ni kilimo na Wilaya ya Meatu ndio wazalishaji namba moja kwa pamba, mpango uliopo ni kwamba kila kijiji kiwe na kiwanda ndani ya Simiyu yaani bidhaa moja kijiji kimoja kwa hiyo ziara yako inaenda sambamba na vipaumbele vya Mh Mkuu wetu wa mkoa”. Alisema Kiswaga.
“Kwetu sisi Mheshimiwa Naibu waziri, mkuu wa Mkoa wetu mara nyingi anapozungumza anasema uwe Mkoa wa Simiyu uwe wa kwanza kwenda kwenye uchumi wa kati na huwezi kwenda uchumi wakati ukiwa umeacha watu wenye ulemavu nyuma kwa hiyo sisi kama viongozi maagizo yako ambayo utayatoa mbele yao sisi tutayatekeleza ” Alisema Kiswaga
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mh pius Machungwa alisema alimuomba Naibu waziri huyo kama ikiwezekana mradi wa kitalu nyumba ujengwe kwa kila tarafa ili kuwawezesha watu wenye ulemavu kuw rahisi kushiriki kikamilifu kwa kua jiografia ya Meatu ni kubwa sana.
Kabla ya mkutano huu mh Naibu waziri alianza kupokea taarifa fupi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya pamoja na kutembelea mradi wa ujenzi wa kitalu nyumba ili kujua ni hatua gani Halmashauri ya Wilaya ya Meatu imefikia katika utekelezaji wa mradi huo mwisho Naibu waziri alihitimisha kwa kuongeaa na watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuona baadhi ya waasiriamali wenye ulemavu pamoja na kupata taarifa fupi.
MWISHO.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.