Serikali Mkoani Simiyu imejipanga kuweka mkakati maalum utakaowasaidia wafugaji kutoka kwenye ufugaji wa kuhama hama na kufanya ufugaji wa kisasa na wenye tija.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika kikao maalum cha viongozi wa Serikali, viongozi wa dini, wafugaji, wataalam na wadau mbalimbali wa sekta mifugo kutoka ndani na nje ya mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Bariadi.
Mtaka amesema Mkoa wake umedhamiria kuwatambua wafugaji na maeneo yao na kutoa elimu juu ya upimaji wa maeneo hayo ili yatumiwe kufuga kisasa na kuachana na ufugaji wa kuhama hama kufuata maji na malisho katika mikoa mingine.
“Hatuwezi kuwa Serikali ambayo ina majibu mepesi kwenye mambo ya msingi, lazima tupate majawabu ya wafugaji ndani ya mkoa wetu, tufike mahali ambapo mfugaji kutoka mkoa wa Simiyu hatapigwa faini kwenye mikoa mingine kwa sababu ya kutafuta maji na malisho”amesema Mtaka.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali kupitia Wataalam wa Kilimo na Mifugo watatoa elimu kwa Wafugaji watakaorasimisha maeneo yao, ili wayatumie kupata malisho ya mifugo na kuweka miundombinu muhimu ya mifugo kama vile malambo, majosho na visima katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji na malisho ya mifugo.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.