Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amewataka Viongozi Mkoani humo wasitoe kauli za kukatisha tamaa watumishi walio chini yao ili waweze kutekeleza majukumu yao vema ikiwa ni pamoja na kushiriki kikamilifu katika Agenda ya Mkoa ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda chini ya Kauli Mbiu"WILAYA MOJA BIDHAA MOJA”.Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watumishi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) duniani yaliyofanyika kimkoa Lamadi Wilayani Busega.Mtaka amesema Serikali Mkoani humo ina agenda katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ambayo ni kujenga Viwanda ambavyo malighafi yake yanapatikana hapa nchini.
Amesema Serikali Mkoani imedhamiria kujenga Mkoa utakaoonesha dira katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda, utaotekeleza Ilani ya CCM, Dira ya Taifa,Mpango wa Taifa wa Miaka mitano, utakaotekeleza maono na matamanio ya Mhe Rais na ili kutekeleza yote haya Viongozi wanahitaji kuungwa mkono na watumishi wa Serikali.“Sisi kama Mkoa tunahitaji kujenga Mkoa wetu kuwa mkoa wa Viwanda kwa vitendo siyo kwa maneno, ili tuweze kujenga uchumi wa Viwanda ni lazima tuungwe mkono na wafanyakazi, ili tuungwe mkono na wafanyakazi ni lazima kauli zetu ziweze kujenga morali kwa wafanyakazi; hauwezi ukawa unataka kujenga uchumi wa viwanda Simiyu halafu unakuwa ni Mkurugenzi au Mkuu wa Idara mwenye lugha za hovyo kwa wafanyakazi ni vitu visivyowezekana” alisemaAmeongeza kuwa chini ya Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja” Serikali imepanga kuwa Wilaya ya Busega iwe na kiwanda cha kutengeneza Tomato sauce,Chilli Sauce na bidhaa zote za mbogamboga ambazo zitauzwa katika mikoa ya Mwanza,Mara,Geita,Shinyanga, Kagera, Singida, Kigoma na Dar es Salaam.Aidha amesema katika wilaya ya Itilima zitatengenezwa sabuni za maji,unga na za miche, wilaya ya Maswa Halmashauri itapata mkopo wa shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki na wilaya ya Meatu itapata shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kupanua kiwanda cha maziwa ili maziwa ya unga yazalishwe pia. Soma zaidi......
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.