Na Linus R. James
Halmashauri ya wilaya ya Meatu imezidi kujiimarisha kudhibiti wimbi la uvamizi wa tembo katika vijiji 22 vinavyopakana na maeneo ya hifadhi za wanyamapori.
Hayo yamebainishwa jana jioni wakati wa makabidhiano ya vifaa mbali mbali vilivyotolewa na shirika la Friedkin Conservation fund (FCF) yaliyofanyka katika ofisi ya Kitengo cha wanyamapori Meatu.
Akibainisha vifaa mbali vilivyotolewa Afisa Wanyamapori Wilaya ya Meatu Bw. Revocatus Meney alisema
“Vifaa hivi ni maalum kwa ajili ya kudhibiti tembo wanaovamia maeneo ya vijiji hasa nyakati za usiku, kwa hiyo vitaongeza ufanisi wa kudhibiti wanyama hawa kabla hawajaleta madhara kwa wananchi wetu “
Pia Afisa wanyamapori huyo alibainisha kuwa jitihada hizo ni mwendelezo wa juhudi za serikali ya awamu ya tano ambapo Mei 20 mwaka huu Jumla ya tembo 18 walifungwa mikanda maalumu yenye vifaa vya GPS kufuatiliaa mienendo yao ndani na nje ya maeneo ya hifadhi.
Vifaa ivyo vyenye takribani thamani ya milioni nne za Kitanzania ni Tochi zinazotoa mwanga maalum (light annoyance) 6, Vipaza sauti maalum 18, mabomu ya pili pili ( Chill bombs) 700 na fataki ( roman Candles) 8 vinatarajiwa kugawanywa katika vijiji kwa vikundi vya vijana vya kudhibiti tembo vilivyoundwa na kitengo cha wanyamapori cha Wilaya.
Afisa wanyapori huyo alichukua nafasi hiyo kumshukuru Bibi Nana Grosse Woodley ambaye ni Afisa mahusiano wa shirika la Friedkin Conservation Fund ambaye amekua mstari wa mbele kufadhiri miradi mingi ya kupunguza migogoro kati ya binadamu na tembo.
Pia shirika la Friedkin Conservation fund (FCF) kwa kushirikiana na shirika la Honey Guide Foundation pamoja ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya tayari wameandaa mafunzo maalum kwa vijana 22 kutoka katika kata zinazoathiriwa na uvamizi wa tembo.
Mafunzo hayo ya siku 11 yanatarajiwa kutolewa kuanzia tarehe 15 mwezi huu katika hifadhi ya wanyamapori ya Jamii ya Randline iliyopo Monduli Arusha.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.