Na Linus R. James ( Meatu DC)
Wilaya ya Meatu mapema leo imetumia kikao kazi cha tathmini ya ugawaji wa vitambulisho vya ujasiliamali pamoja na tathmini ya Mwenge wa uhuru 2019 kilichohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa wilaya yaan Mkuu wa Wilaya Dr. Joseph E. chilongani, Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Fabian Manoza, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Pius Machungwa,, Wah madiwani pamoja na wajumbe wa kamati mbali mbali za kudumu za halmashauri kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, watendaji wa kata na vi.jiji, ma afisa kilimo na mifugopamoja na Maafisa elimu, wakuu wa shule , walimu wakuu pamoja na watumishi wote wa makao makuu kuimarisha mahusiano na kuhakikisha vitambulisho vinagawiwa kwa kasi.
Akifungua kikao kazi mapema leo katika ukumbi wa Halmashauri kilichokua na agenda mbili yaani tathimini ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali na Tathmini ya mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru Dr. Joseph e. Chilongani alisistiza wataalam, viongozi wa chama, Wah madiwani kuzidi kutoa elimu kwa wananchi wa Meatu ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa, kuhusu manufaa ya kuwa na vitambulisho vya ujasiliamali.
Mkuu wa Wilaya huyo amewatakwa wajumbe kuhakikisha wanakua wamoja kuhakikisha wanawaelimisha wananchi manufaa ya kuwa na vitambulisho ili kuhakikisha wajasiliamali wote wanapewa vitambulisho.
“Tatizo lilikua kwamba watu wengi hawajapata elimu ya wajasiliamali, uongozi ni kuongoza njia iliyo nzuriivyo tuhakikishe tunawaongoza watu kwa kufuatasheria bila shuruti kwa manufaa yao” Alisema Dr. chilongani.
Mkuu wa wilaya huyo alisistiza kuwa lengo si tu kumaliza vitambulisho bali ni kuhakikisha kuwa wajasiliamali wote wanafikiwa.
Katika Suala la mbio za Mwenge Mku wa Wilaya amewapongeza wajumbe kwa ushirikiano waliouonesha kuhakikisha mwenge unapokelewa na miradi yote inakubaliwa na mWenge wa uhuru.
Ivyo Mkuu wa Wilaya alisisitiza kuwa umoja uliooneshwa uendelee kuimalika si tu kwenye vitambulisho bali katika mambo yote yanayolenga kuleta maendeleo katika Wilaya yetu ya Meatu.
Naye mkurugenzi Mtendaji Ndg. Fabian Manoza akipokea takwimu ya ukusanyaji wa vitambulisho kwa makundi(timu) mbali mbali alisema
“Nikiwemo mimi Mkurugenzi Mtendaji, Mkuu wa Wilaya, mwenyekiti wa halmashauri, katibu tawala wa Wilaya tuna chukua kitambulisho kimoja kimoja kuhakikisha na sisi tunaenda kuwapatia wajasiliamali ili na sisi kama viongozi tushiriki ili zoezi la kugawa vitambulisho”.
Suala la mkurugenzi kuongoza viongozi wenzake kuchukua kitambulisho liliweza kugusa mioyo ya Wah madiwani ambapo nao wameomba wafanye kama viongozi walivyochukua hatua ya kuchukua kitambulisho kwenda kugawa.
Kikao kimeazimia kila mshiriki achukue kitambulisho kimoja kimoja na ahakikishe anamtafuta walau mjasiliamali mmoja na anamgawia ili walau kila mshiriki awe sehemu ya ushiriki wa ugawaji wa vitambulisho vya uasilimali.
Akizungumza kwa niaba ya madiwani mwenyekiti wa halmashauri wa Wilay alisema suala la kuchukua kitambulisho kimoja ni zuri sana lakini kwa sisi madiwa ni tuna kata ambazo zina Zaidi ya kijiji kimoja ivyo alisisitiza madiwani wenzake walau wajitahidi kutafuta mjasiliamali mmoja kila kijiji suala ambalo limeungwa mkoo na Wah madiwani waliohudhuria.
Wakichangia kwa nyakati mbali mbali, Wah madiwani wameonekana kufurahishwa na kikao hicho ambapo wamesisitiza kuwa vikao kama ivi ni muhimu kwa vinaimarisha ushirikiano katika Wilaya ya Meatu.
Jumla ya vitambulisho 8,642 katika Wilaya ya Meatu vimeshagawiwa katika wajasiliamali kati ya vitambulisho 11,000 vilivyotolewa.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.