MEATU MABIGWA NYAKABINDI
Na Benton Nollo, Nyakabindi Bariadi
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu imeibuka mshindi kwa kushika nafasi ya Kwanza katika Kundi la Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (maarufu kama Nane Nane) Kanda ya Ziwa Mashariki mwaka 2022 ambayo yamehitimishwa tarehe 08 Agosti 2022.
Akisoma taarifa ya Kamati ya Ushindanishaji na Tathmini ya Maonesho ya Nane Nane 2022, Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Nane Nane Kanda ya Ziwa Mashariki, Beda Chamatata ameeleza kwamba Halmashauri hiyo imepata alama 95.08 na kuzishinda Halmashauri zote 21 za Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.
Halmashauri hizo zilishindanishwa katika maeneo matatu ambayo ni mabanda, vipando na mifugo ambapo wastani wa alama katika sehemu hizo ndiyo uliotumika kutoa mshindi wa kwanza hadi wa tatu.
Halmashauri nyingine zilizopata ushindi ni Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Sinyanga ambayo imeshika nafasi ya pili kwa kupata alama 86.10 na Halmashauri ya Mji Bariadi mkoani Simiyu ambayo imeshika nafasi ya tatu kwa kupata alama 80.58.
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu inashika nafasi ya kwanza kwa mara ya tatu mfululizo.
Mbali na ushindi huo, Halmashauri ya Wilaya ya Meatu pia imeshika nafasi ya pili katika mshindi wa jumla kwenye maonesho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja wa Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya Ajenda 10/30 Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda.
Matukio katika Picha:
Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane 2022, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda (wa kwanza kushoto aliyevaa Skafu) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee (wa pili kushoto) kwa pamoja wakimkabidhi kombe Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Meatu, Thomas Shilabu (wa kwanza kulia) baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kushika nafasi Kwanza katika Kundi la Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye Maonesho hayo yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022 yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane 2022, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda (wa pili kushoto aliyevaa Skafu), Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee (wa tatu kushoto) na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga (wa kwanza kushoto) kwa pamoja wakimkabidhi kombe Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Meatu, Thomas Shilabu (wa kwanza kulia) baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kushika nafasi Pili katika nafasi ya mshindi wa jumla kwenye Maonesho hayo yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022 yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Nane Nane Kanda ya Ziwa Mashariki mwaka 2022, Beda Chamatata akisoma taarifa ya Kamati ya Ushindanishaji na Tathmini ya Maonesho ya Nane Nane 2022, wakati wa sherehe ya kuhitimisha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane 2022, yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu tarehe 08 Agosti 2022 ambapo Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda. Maonesho hayo yalianza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Msoleni Dakawa (aliyevaa suti ya kijivu katikati) akisherehekea ushindi pamoja na baadhi ya Watumishi na Wajasiriamali walioshiriki Maadhimisho ya Wakulima Nane Nane 2022, yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu yaliyoanza tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022. Ambapo Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura akipiga makofi kwa furaha baada ya Halmashauri yake kutajwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa Mashariki, Beda Chamatata (hayupo pichani) kuwa imeshika nafasi ya Kwanza katika Kundi la Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye Maonesho hayo yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022 yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Ziwa Mashariki 2022, Dkt. Yahaya Nawanda (hayupo pichani) Beda Chamatata (hayupo pichani) wakati wa kilele cha maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022.
Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane 2022, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda (aliyevaa Skafu) akimsikiliza Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Meatu, Thomas Shilabu (wa pili kulia) wakati akikagua vipando kwenye banda la kilimo la Halmashauri hiyo yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022.
Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane 2022, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda (aliyevaa Skafu) akitoka akikagua vipando kwenye banda la kilimo la Halmashauri ya Wilaya ya Meatu yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022.
Muonekano wa bidhaa na vipando mbalimbali zilizozalishwa na kustawishwa kwenye Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane 2022, kwenye banda la kilimo la Halmashauri ya Wilaya ya Meatu katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Msoleni Dakawa pamoja na baadhi ya wananchi wakiwa kwenye banda la Halmashauri hiyo lenye bidhaa mbalimbali za Wajasiriamali katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane 2022, yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti 2022 na kuhitimishwa tarehe 08 Agosti 2022.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.