Na Linus R. James ( MEATU DC)
Hayo yamebainishwa jana jioni katika kikao cha maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2019 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
Kikao hicho kilichoongozwa na Mh Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dr. Joseph E. Chillongani kilikua na wajumbe mbali mbali ambao ni pamoja na, kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, Viongozi wa Chama tawala wa Wilaya, Mkurungenzi Mtendaji Ndg, Fabian Manoza Said, Wakuu wa Idara mbali mbali wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na taasisi mbalimbali, viongozi wa dini mbali mbali pamoja na wadau wa maendeleo wa wilaya, kililenga kujadili namna nzuri ya kuukaribisha na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru ndani ya Wilaya.
Licha ya kupendekeza njia na miradi ambapo mwenge wa Uhuru utapita kwa lengo la kukakua au kuweka jiwe la msingi au kufungua, Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii iliweza kukitambulisha kikundi cha vijana kiitwacho “ Meatu Leather Product” .
Aidha kiongozi wa kikundi hicho aliweza kutambulisha bidhaa mbali mbali ambazo kwa sasa wanazitengeneza ikiwa ni pamoja na mafuta ya kupaka, sabuni na batiki. Aidha waliweza kuonesha sampuli za batiki walizozitengeneza kwa mikono yao wenyewe ambapo wajumbe waliweza kuchagua na kupendekeza batiki zao ziwe ndiyo sale rasmi ya Mwenge wa Uhuru.
Naye Mkurugenzi mtendaji Ndg. Fabian Manoza Said akitoa ufafanuzi wa kikundi hicho alsema licha ya kwamba jina la kikundi limebeba bidhaa zitokanazo na ngozi alisema kikundi hiki kimeanza kutengeneza batiki kwa sababu bidhaa ya ngozi inahitaji uwekezaji mkubwa na kwa sasa halmashauri ya Wilaya ya Meatu haipo vizuri sana kifedha.
“Wakatii naletewa ikundi kwa ajili ya kuomba 4% wazo la batiki halikuniingia akilini, nilimwambia afisa maendeleo anitafutie kikundi kinachojishughulisha na ngozi kwa sababu ngozi ni ‘hot cake’ kwa sababu mifugo tunayo ya kutosha, lakini baadae tulipata hiki kikundi cha uzalishaji wa bidhaa za ngozi, hata ivyo mtaji wa ngozi ni mkubwa na watahitaji mafunzo ” Alisema Mkurugenzi.
Mkurugenzi alisisitiza kuwa kikundi kikipata mtaji na tenda ya mwenge kitaweza kuanza kuzalisha bidhaa za ngozi na ivyo kukamilisha hadhima kuu ya uanzishwaji wa kikundi hiki cha " Meatu Leather Product".
Naye afisa maendeleo wa Wilaya Bi Mwanaisham Nassor alisisitiza kuwa, hizi ni jitihada za kuendeleza sera ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati na viwanda pamoja na kuwainua vijana.
“ Tayari Ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara yetu imeshatoa aslimia nne kwa hiki kikundi na kikundi kimepewaa mafunzo ya batiki kutoka kwa mtaalam aliyetoka geita, kikundi kinaweza kuzalisha vipande visivyopungua 100 kwa siku”. Alisema Bi Mwanaisham.
Mwisho
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.