Na Linus R. James
Mbio za mwenge wa uhuru Wilayani Meatu zimeonekana kuwafurahisha wananchi pamoja na viongozi wa Wilaya ya Meatu,
Kwa mwaka 2019 Mwenge wa Uhuru umepitia miradi 5 yenye thamani ya Tshs. 1,582,459,370.00 ambayo imechangiwa na wadau mbalimbali yaani Serikali Kuu Tshs. 70,227,470.00, Halmashauri ya Wilaya Tshs.51,670,600.00, Wananchi 746,991,300.00 na Sekta binafsi ni Tshs.80,570,000.00.
Katika Miradi hiyo Mwenge wa Uhuru Umekagua mradi wa Maji wa itinje na kupanda miti, umekagua kitalu cha mbegu bora ya zao la pamba Katika kata ya Mwabusalu,umezindua vyumba 2 vya maabara ya Kemia na biologia katika shule ya Sekondari Mwandoya, umezindua klabu ya Mapamabano dhidi ya rushwa na Klabu ya kupambana mimba za Utotoni, umefungua Nyumba ya kulala wageni(TS Lodge), pamoja na kukagua mradi wa wajasiliamali ( Meatu Leather Product).
Naye kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ali pamoja na timu yake wameridhia miradi yote kama ilivyopendekezwa na uongozi wa Wilaya ya Meatu kwa niaba ya Wananchi hali iliyoonekana kuleta furaha kwa wananchi pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu waliojitokeza katika mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mbali na Kuridhia miradi hiyo Kiongozi amefurahishwa na ubunifu wa miradi hususani klabu ya kupambana na mimba ya utotoni, kitalu cha uzalishaji wa pamba, Nyumba ya Kulala wageni pamoja na kikundi cha wajasiliamali
“ Tangia tumeanza mbio za Mwenge Mkoani Songwe hatujawahi kukutana na klabu za namna hii ya mapambano dhidi ya mimba za utotoni”. Alisema Mzee Mkongea
Akisoma Risala ya Utii mble ya Kiongozi wa mbio za Mwenge katibu tawala wa Wilaya ya Meatu Ndg. Albert Rutahiwa alisema Sisi wananchi wa Wilaya ya Meatu kwa dhati na furaha kubwa tumeupokea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru usemao “Maji ni Haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa” na kauli mbiu isemayo “pima, jitambue , ishi”, “Kataa rushwa, Jenga Tanzania”, “Tujenge maisha yetu, Jamii na Utu wetu bila dawa za kulevya” na “Nipo tayari kutokomeza Malaria, wewe Je?” Alisema Ujumbe huu wa mbio za mwenge wa Uhuru unazingatia hoja, Vipaumbele, Mikakati, dhana ya ushirikishwaji wa Wananchi katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya Maji na kuwakumbusha kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Baada ya kusikiliza risala ya Utii kiongozi wa mbio za Mwenge amekagua mabanda mbali mbali ambayo ni banda la TAKUKURu Meatu, Banda la mapambano dhidi ya madawa ya Kulevya Meatu, banda la uchaguzi, banda la wajasiliamali mbali mbali wanauza bidhaa pamoja na banda la afya.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilayani Maswa ambapo umeipitia miradi mbali mbali, utafanya mkesha katika mji wa Mwanhuzi kisha kesho utakabidhiwa katika kijiji cha Gambatinga Wilaya ya Itilima
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.