Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Elimu hususani ya juu ni nguzo Muhimu ya kufikia Agenda ya Serikali ya kuwa na Tanzania ya Viwanda na kufikia Uchumi wa Kati ifikapo 2025.
Makamu wa Rais wa amesema hayo, wakati wa akifungua kongamano la elimu ya juu na Tanzania ya viwanda lililofanyika mjini Bariadi. Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo kikuu huria Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Amesema kutokana na umuhimu huo Serikali imeamua kuwekeza katika Elimu na Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025 imeweka elimu kuwa kipaumbele cha juu kwa kuwa ndiyo kitovu cha kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii.
“Ninyi ni mashahidi kuwa Serikali imeweka mkazo kwenye elimu, tumeanza na shule za msingi, sekondari lakini pia tumeongeza bajeti kubwa kwenye mikopo ya Elimu ya Juu na tutakwenda polepole mpaka tuhakikishe Watanzania wanapata elimu ya kutosha ili kuendana na uchumi wa Viwanda” alisema Makamu wa Raisi.
Ameongeza kuwa lengo kuu la Serikali ni kuongeza kipato cha wananchi kupitia viwanda ambavyo vitaongeza thamani ya mazao yanayozalishwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.Soma zaidi...
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.