• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Meatu District Council
Meatu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Halmashauri ya Wilaya ya Meatu

  • Mwanzo
    • sub home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Core Values
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Miundombinu, Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Pre Primary Education
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango na Uratibu
      • Utumishi, Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Maliasili na Utunzaji wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha
      • Uratibu wa Manunuzi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji na Uvuvi
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Fishing
    • Expertise
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao
      • Fedha, Uongozi na Mipango
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha habari

Maelekezo 7 ya Waziri Mkuu Majaliwa Kuimarisha Ulinzi Rasilimali za Uvuvi Nchini

Imewekwa: November 17th, 2022

Na Benton Nollo, Mwanza

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb) ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Viongozi, Watendaji wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanashirikiana kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha ulinzi wa rasilimali za uvuvi na kutokomeza uvuvi haramu ili sekta ya uvuvi iendelee kutoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (Mb) alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waziri Mkuu na Watendaji wa Serikali na Wadau wa Uvuvi wa Kanda ya Ziwa Viktoria uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.

Kupitia mkutano alitoa maelekezo kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekta binafsi kwa maana ya Wavuvi, Wenye Viwanda, Wafanyabiashara ya Samaki, Mazao ya Samaki na zana mbalimbali za uvuvi kama ifuatavyo;

Kwanza, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ihakikishe inaandaa mikutano ya mara kwa mara itakayokutanisha wadau wote muhimu wa uvuvi kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu changamoto mbalimbali za sekta ya uvuvi na kuzitatua hususan suala la uvuvi haramu.

Pili, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji kote nchini kuhakikisha kuwa vitendo vya uvuvi haramu vinakomeshwa katika maeneo yao na wote watakaopatikana na makosa ya uvuvi haramu wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sharia.

Tatu, alisema kwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya mapato vya OR-TAMISEMI ni shughuli za uvuvi, kila Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama kuhakikisha hakuna vitendo vyovyote vya uvuvi na biashara haramu kwenye eneo lake.

Nne, Waziri Mkuu aliagiza kila Mkurugenzi wa Halmashauri ahakikishe anatenga na kurudisha asilimia 5 ya mapato yanayotokana na sekta ya uvuvi ili kuimarisha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi kulingana na miongozo iliyopo.

Tano, Watendaji wote wa serikali watakaothibitika kupokea rushwa kutokana na vitendo vya uvuvi na biashara haramu ya mazao ya uvuvi wa aina yoyote ile watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi.

Sita, alitoa wito kwa wavuvi na wadau wa uvuvi nchini kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria na kanuni za uvuvi pamoja na sheria nyingine za nchi huku akionya kuwa atakayekamatwa anafanya vitendo vya uvuvi haramu atachukuliwa hatua za kisheria hapo kwa hapo kwa kuwa serikali haitavumilia tena vitendo hivyo.

Saba, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI waendelee kutoa elimu kwa umma kuhusu ulinzi na usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi.

Aidha Waziri Mkuu aliongeza kuwa, kuanzia sasa, pamoja na majukumu mengine, suala la usimamizi na ulinzi wa rasilimali za uvuvi litatumika kupima utendaji wa kazi wa viongozi hao huku akiwataka kuhakikisha kwenye utoaji wa taarifa za utekelezaji wa majukumu yenu suala la usimamizi na ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika taarifa za mwezi, robo mwaka na mwaka linajumuishwa na kujidhihirisha ipasavyo.

Mkutano huo wa siku mbili kuanzia Novemba 17-18, 2022 umelenga kujadiliana na kuweka mipango ya kusimamia, kulinda na kuendeleza sekta ya uvuvi ili iendelee kutoa mchango wake katika utoaji wa ajira, chakula na lishe, kipato na pato la Taifa kwa ujumla.

Matukio katika Picha:

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (Mb) akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waziri Mkuu na Viongozi wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Viktoria uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (Mb) akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (Mb) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Waziri Mkuu na Viongozi wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Viktoria uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah akitoa wasilisho kuhusu Hali ya Sekta ya Uvuvi nchini katika  Mkutano wa Waziri Mkuu na Viongozi wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Viktoria uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda (wa pili kushoto) akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb) iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (Mb) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waziri Mkuu na Viongozi wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Viktoria uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Prisca Kayombo (katikati) akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb) iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (Mb) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waziri Mkuu na Viongozi wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Viktoria uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.

Mkuu wa Meatu, Fauzia Ngatumbura (aliyevaa kilemba chekundu) akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb) iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (Mb) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waziri Mkuu na Viongozi wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Viktoria uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Msoleni Dakawa (aliyevaa miwani kushoto) akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb) iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (Mb) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waziri Mkuu na Viongozi wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Viktoria uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.

Sehemu ya washiriki wakiwa  katika Mkutano wa Waziri Mkuu na Viongozi wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Viktoria kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza tarehe 17 Novemba 2022.


Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi September 16, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji kwa Ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa September 16, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 20, 2024
  • Taarifa ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Matokeo ya Mwanzo February 20, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi Karibuni

  • Jamii Yatakiwa Kupinga Mila Potofu, Kandamizi

    March 08, 2023
  • Meatu Pikipiki Tisa

    February 14, 2023
  • TAKUKURU RAFIKI

    January 27, 2023
  • Hongereni Wataalam: Ngatumbura

    January 27, 2023
  • Angalia zote

Video

Ziara ya Waheshimiwa mawaziri nane Wilaya ya Meatu kwa ajili ya kukusanya Maoni ya Kutatua Migogoro
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Miongozo Mbali mbali
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari
  • Dokumenti mbali mbali

Tovuti mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara ya Takwimu(NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu huria
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Meatu, Simiyu, Tanzania

    Anwani ya Posta: S.L.P 44

    Simu: 028 2795 008

    Simu ya Mkononi: 0622 404 712

    Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.