Na Linus R. James - Meatu DC
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Wilayani Meatu jana yalikua ya shamrashamra kubwa sana ikiwa ni pamoja na burudani mbali mbali kutoka vikundi vya wanafunzi wa Wilaya ya Meatu, Ngonjera na shuhuda mbali mbali.
Maadhimisho hayo yaliyoanza kwa maandamano kutoka viwanja vya stendi ya Mwanhuzi huku yakiwa na vikundi vya bodaboda, wanawake wa Wilaya ya Meatu pamoja na wanafunzi wa shule mbali mbali Mwanhuzi, yamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mh. Dr. Joseph Chilongani pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, viongozi mbali mbali wa taasisi na vyama vya siasa na wakuu wa Idara na vitengo mbali mbali vya Wilaya ya Meatu.
Katika maadhimisho hayo taarifa, shuhuda, na hotuba mbali mbali zimeweza kutolewa ambapo zimeweza kuwa burudisha, kuwakumbusha mambo mbali mbali kugusa wananchi waliohudhuria katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu hususani mambo yanayowahusu wanawake kama kujikwamua kiuchumi, kuweka akiba, msaada wa kisheria n.k.
Moja kati ya shuhuda ambayo imewagusa wananchi ni ile ya mwnafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Lyusa anayefahamika kwa jina la Theresia Ngassa
Akitoa ushuhuda wake mwanafunzi huyo kuhusu jinsi alivyopata changamoto ya kukatazwa kuendelea shule na baba yake mzazi kwa madai ya kwamba akaolewe. Mwanafunzi huyo ambaye alionekana kuelezea kwa uoga huku akilengwa na machozi alishindwa kuendelea na ivyo kumkaribisha Mwalimu Mkuu wa shule ili aendelee kutoa maelezo.
Kwa maelezo yaliyotolewa ilionekana Mwanafunzi huyo anahitaji mahitaji mbali mbali, ivyo kuwafanya wageni walioalikwa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti CCM wilaya kutoa mchango ambapo mbali mbali ya fedha taslim pamoja na vifaa vya shule.
Hata ivyo Meneja wa NMB tawi la Mwanhuzi aliweza kuguswa ambapo ametoa zawadi mbali mbali za vifaa vya shule ikiwemo madaftari, mifuko pamoja na kumfungulia mwanafunzi huyo akaunti benki ya NMB na kumtangaza mwanafunzi huyo kuwa balozi wa NMB katika wilaya ya Meatu.
Idara ya maendeleo ya Jamii kwa kushirikian na madiwani a viti maalum, Mh Mbunge wa Viti maalum Mh Leah Komanyana Umoja wa wanawake wilayani Meatu ulianza wiki ya maadhimisho yake kuanzia tarehe 4 mwezi machi ambapo jumla ya mifuko ya sukari 25 imegawiwa katika shule za mbali mbali za Meatu kwa kushirikiana na Mbunge wa viti maalum Mh. Leah komanya na siku ya kilele wameweza kutoa jumla mifuko kumi ya Unga wa sembe .
Maadhimisho haya ambayo yamebeba kauli mbiu “ Badili fikra kufikia Usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu” kitaifa ambapo kiwilaya ujumbe ulikua “Tokomeza mimba mashuleni na kupandisha ufaulu kwa wsichana”ukiwa na lengo la kupandisha ufaulu hususani wasichana wa Wilaya ya Meatu.
Akifafanua ujumbe huo Afisa Maendeleo(W) meatu Bi Mwanaisham Nassor alitoa takwimu za mimba ambapo kwa shule za sekondari mwaka 2015 ni mimba 5, 2016 mimba 20, 2017 mimba 242018 mimba 15 na 2019 mimba 2019 na kwa upande wa elimu msingi kwa 2015 ni mimba 1, 2016 mimba 3, 2017 mimba 4, 2018mimba 8 na 2019 ni mimba 0 ambapo alihitimisha kuwa mapambano haya yatakua ni endelevu kuhakikisha mimba zinatokomezwa na kiwango cha ufaulu kinapanda.
Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa mgeni rasmi Dr. Joseph Chilongan kutoa hotuba fupi na kisha kugawa zawadi kwa akina mama na wanafunzi mbali mbali waliofanya vizuri( Mama Shupavu) ndani ya Wilaya.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.