Na Linus R. James( Meatu)
“Kama kuna jambo lolote baya basi Serikali yetu ya Magufuli haiwezi kuthubutu kulileta kwa wananchi”. Hayo yamesemwa na Mh Mkuu wa Wilaya Dk. Joseph Chilongani katika uzinduzi wa chanjo ya kansa ya shingo ya kizazi katika Wilaya ya Meatu.
“Hili sio jambo la kuzuia uzazi bali ni kuzuia ugonjwa unaotokana na uzazi” aliongeza Chilongani. Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya huyo aliwapongeza watumishi wa Wilaya ya Meatu, makundi mbali mbali ikiwemo makundi ya wawakilishi wa dini, vyama vya siasa na waratibu wa mradi wa chanjo.
Aliwahimiza waendelee kulitangaza hili suala kwa mtazamo chanya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutumia lugha njema na kutanguliza uzalendo wakati wa kutoa huduma.
Awali akifungua zoezi kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Dk. Adam Jimisha alitoa taarifa fupi ya chanjo ambapo alisema kuwa Chanjo hii ni endelevu na ni zoezi la kitafa.
Kaimu Mganga Mkuu alisema kuwa chanjo hii haina madhara yoyote kwani imefanyiwa majaribio mbalimbali na shirika la afya duniani (WHO) ambapo hapa nchini majaribio yamefanyika katika mkoa wa Kilimanjaro. Pia alisema zoezi hili ni la kitaifa na lilizinduliwa rasmi Mkoa wa Dar es salaam tarehe 10/04/2018 ambapo kwa Wilaya ya Meatu jumla ya wasichana 11966 wanatarajiwa kupewa chanjo kwa mwaka. Pia alisema kuwa chanjo hii itatolewa bure katika vituo vya afya kwa awamu mbili yaani awamu ya kwanza na awamu ya pili ni baada ya miezi sita tangu msichana atakapochomwa chanjo ya kwanza.
Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ndugu Gervas Amata wakati akimkaribisha mwenyekiti wa Halmashauri alisisitiza kuwa suala hili limekuja wakati muafaka kuokoa vifo kwa wanawake.
“ Wakina mama ndio kila kitu, ndio wazazi, walezi lakini wakina mama ndio walimu na washauri wa mambo yetu katika ngazi ya familia na jamii, tukiokoa wakina mama tumeokoa taifa” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Gervas Amata.
Aliwahimiza wananchi kuwa wananchi wakiacha na kulipuuza zoezi hili matokeo yake siku za baadaye tutapoteza wanawake kwa vifo mbali mbali itakayopelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Pius Z Machungwa alisema kuwa chanjo hii katika Wilaya ya Meatu itakua msaada mkubwa katika kujenga afya za wakazi hususani wanawake ambapo pia alihimiza kuwa hili sio jambo baya na chanjo haina madhara kwa wananchi hivyo aliwasihi wazazi wawaruhusu watoto wao wajitokeze kwa wingi kupata chanjo.
Zoezi hili lilitanguliwa na maandamano ya wanafunzi kutoka shule za serikalini nne na binafis moja ambazo ni Mwanhuzi shule ya msiingi, Mshikamano shule ya msingi, Panaeli shule ya msingi Kimali Sekondari na Meatu sekondari na yalihitimishwa katika viwanja vya Mwanhuzi S/M.
Kama ishara ya uzinduzi Mh Mgeni rasmi ndugu Chillongani alikata utepe na baadhi ya wasichana walipewa chanjo mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa.
Aidha zoezila chanjo lilianza kutolewa sambamba katika hospitali ya Wilaya jengo la RCH na litakua ni endelevu kwa wasichana kuanzia miaka tisa lakin kwa kuanza litaanza na wenye umri wa miaka 14 maelekezo mengine yatatolewa kwa wananchi hapoa baadae.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.