Na Benton Nollo, Mwanhuzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Msoleni Dakawa amesema Serikali inategemea matokeo chanya yatakayotokana na utafiti wa Gesi ya Helium katika Bonde la Ziwa Eyasi.
Dakawa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wataalam wa Mazingira kutoka Kampuni ya Paulsam Geo-Engineering waliofika ofisini kwake mapema leo tarehe 24 Januari 2023 kwa ajili ya kujitambulisha na kupata kibali cha kufanya tathmini ya athari ya mazingira kwa ajili ya kufanya utafiti huo.
Kampuni ya Paulsam Geo-Engineering (Paulsam Geo-Engineering Company Limited) ndiyo iliyoshinda zabuni ya kufanya tathmini ya athari ya mazingira kwa ajili ya kufanya utafiti huo ambao utafanywa na Kampuni ya Noble HELIUM kupitia Kampuni tanzu ya Tanzania ya Antares Limited.
Kampuni ya Antares inatarajia kufanya utafiti wa Gesi ya Helium katika Bonde la Ziwa Eyasi ambapo kwa Wilaya ya Meatu Kata itakayohusika na utafiti huo ni Bukundi katika Vijiji vya Lukale na Mwabagimu.
Utafiti huo unatarajiwa kufanyika wakati wa kiangazi kikali yaani mwezi Septemba hadi Novemba 2023.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.