Na Linus R. James - Meatu
Mkurugenzii Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ndugu Fabian Manoza amewahimiza wafanyakazi wa sekta ya afya kujituma katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni njia ya kuimarisha huduma hiyo pamoja na kuwezesha kufanya vizuri katika miradi mbali mbali inayoendelea ndani ya Wilaya.
Akizungumza mapema ndugu Manoza leo hii katika ufunguzi wa mafunzo ya huduma ya afya ya mfuko wa jamii CHF iliyoboreshwa) amehasa wenyeviti wa kamati za afya katika ngazi ya zahanati na vituo vya faya kuwa wawe makini na waadilifu wakati wanatekeleza miradi yao pamoja hasa kuisimamia kuhakikisha kuwa inakua ni ya kuleta tija katika jamii yao.
“Pesa zote zinazolenga uboreshaji wa afya kwa ngazi ya kijiji, zinaletwa kwenye zahanati lakini wenyeviti mmeshindwa kuzisimamia, sasa ivi mnaingiziwa pesa za basket, pesa za RBF, pamoja na CHF, pesa zote mnazo nyinyi lakini wenyeviti kusema mkae vizuri na kamati zenu mtengeneze mipango mizuri bado hamjaweza kufanya ivo” Alisema Manoza.
Aliwasistitiza kuwa mda wanapokosa pesa wanalalamika lakini zinapoletwa wanashindwa kuonesha matokeo mazuri kwa wananchi.
“Kwa hiyo mimi niwatake mwende mkarekebishe kasoro zinazojitokeza, kinyume cha hapo serikali itaona hakuna maana ya kuleta pesa” Alisisitiza mkurugenzi
Naye katibu tawala wa Wilaya Bi Veronica S. Kinyemi aliwasisitiza washiriki kuwa makini wakati wa mafunzo ili wapate uelew na wakalete ufanisi kwenye vituo vyao.
”Hapa ni makao makuu ya wilayapana mambo mengi sasa isiwe badala ya kuhudhuria mafunzo wewe kila saa na simu nje, mara unaenda benki mara sijui kuonana na nani kiasi kwamba haya mafunzo usiyapate kama yalivyotarajiwa” Alisema Bi Veronica
Akifungua mafunzo, Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dk. Joseph Chilongani alisema kuwa yeye ni dokta(mtabibu) kwa taaluma na kuwaambia kuwa anaelewa machungu ya mgonjwa anapoenda kupata huduma ya matibabu.
“Mimi niseme mmekuja kwenye CHF inayoboreshwa kwa sababu hii iliyopo haijafanya vzuri ivyo tunataka CHF inayofanya vizuri” Alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Aliwahimiza pia kuacha mazoea na wabadilike wafanye kazi kwa weledi ili kuhakikisha huduma inayotarajiwa kwa wananchi ipatikane ambapo pia alitoa maagizo kuwa zahanati amabazo hazifanyi kazi zishughulikiwe haraka ili wananchi wapate huduma ya afya iliyoboreshwa.
“Unaweza ukaugua ukajikuta mfukoni huna pesa lakini kama una bima utahudumiwa kwa sababu tayari ulishachangia” Alidokeza.
Lakini aliwahimiza wenyevti kusimamia kwa ufanisi kuboresha huduma ili wananchi wahamasike kujiunga na bima ya afya.
Mafunzo hayo ya CHF iliyoboreshwa ambayo katika Wilaya ya Meatu yameanza leo kwa ngazi ya Zahanati, vituo vya afya na hospitali yanatarajiwa kuchukua siku tatu yakifuatiwa na mafunzo ngazi ya vijiji ambapo yatahusisha maafisa wasajiri(enrollment officers) ambao watachaguliwa katika jamii kulingana na mwongozo uliotolewa,aidha yatafuatiwa na ufundishaji pia katika ngazi ya vijiji kwa maafisa usajili watakaoteuliwa kulingana namwongozo uliotolewa.
Aidha baada ya ufunguzi huo mkurugenzi wa Wilaya liambatana na wakuu wa Idara mbali mbali za Wilaya hiyo kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa ikiwemo uboreshaji wa Hospitali ya Wilaya unaohusisha ujenzi wa maabara, chumba cha upasuaji“theater” pamoja na wodi ya wazazi, piaa kukagua ukarabati wa zahanati.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.