Na Linus R. James - MEATU DC
Mkuu wa wilaya ya Meatu Dk. Joseph E. Chilongani ameongoza hafla ya kuwapongeza wahitimu katika kituo cha elimu ya watu wazima ngazi ya stashahada kituo cha Meatu iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu jana jioni.
Dk Chilongani ambaye alikua mgeni rasmi wa hafla hiyo alionekana kufurahishwa sana na tukio hilo ambapo alisema ni jambo jema sana la kihistoria tangu kuanzishwa kwa wilaya ya Meatu.
“ Nyinyi mmekua chachu nzuri katika Wilaya yetu mnaona watu wamekuja na familia zao leo na nisingependa mkomee hapa, ningependa muendelee elimu ya juu Zaidi” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Pia mkuu wa wilaya alisema kuwa kukosa majengo haimaanishi mambo hayafanyiki ambapo aliahidi kushirikia na Idara ya elimu ili kufanya mazungumzo ya kuwa na kozi nyinginezo ikiwa ni pamoja na shahada..
“Fursa ya kujiendeleza ipo kama mnavyojua nchi yetu inatusisitiza maendeleo ya viwanda, maendeleo ya uchumi, na haya yote hayaji pasipokkuwa na wasomi”. Alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mtendji wa Wilaya ya Meatu Ndg. Gervas Amata alisema kuwa kwa kuwa mtu anapopiga hatua nyingine ya kielimu anahitaji stahiki ikiwa ni pamoja na mishahara na vituo vya kazi alimwambia mgeni rasmi kuwa stahiki hizo zitatekelezwa kwa mujibu wa utarabibu na ofisi yake itajitahidi kuzifanyia kazi changamoto mbali mballi zinazojitokeza katika kituo hicho cha elimu ya watu wazima.
Naye mkuu wa Idara ya Elimu Ndg. Mshana Kawia akimkaribisha mgeni rasmi licha ya kumshukuru mkurugenzi mtendaji kwa kukubali kituo kianzishwe na kutoa chakula kipindi chote cha masomo aliweza kubainisha mikakati iliyopo katika kituo hicho ambapo alisema kituo kina mkakati wa kutoa elimu ngazi ya shahada kwa kipindi cha baadae. Pia alibainisha faida ambazo wanazipata wanafunzi wanaosoma katika Kituo cha elimu ya watu wazima hususani walimu,
“ Kituo hiki kina faida kubwa kwa sababu kwanza walimu hawa wanasoma kipindi cha likizo, kwa hiyo walimu wanapata mda wa kufundisha, kutunza familia zao na kufanya shughuli za ujasiriamlai”. Alisema Ndg. Mshana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu chini ya Idara ya Elimu msingi katika Jitihada za kuboresha taaluma ya walimu ilianzisha kituo cha stashahada ya elimu ya watu wazima mnamo mwezi Disemba 2016 ambapo kituo kilifunguliwa rasmi na mkurugenzi mtendaji tarehe 10/04/2017 ambapo kilianza na wanafunzi 32 wote wakiwa ni waalimu wa shule mbali mbali wilayani meatu ambapo mwaka 2019 wanafunzi 29 wamehitimu masomo yao.
Akisoma risala kwa niaba ya Wahitimu mwanafunzi alisema kuwa kati ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na walimu kuongeza umahili kazini
“Moja ya mafanikio ya kituo cha elimu ya watu wazima hapa Meatu ni kuwepo kwa wahitimu wapatao 29 wenye diploma ya elimu ya watu wazima, kwa hiyo Idara ya elimu imeongeza watumishi wenye umahiri wa kutosha” alisema muhitimu
Kituo hiki kinakabiriwa na changamoto mbali mbali zikiwemo kutokua na majengo yake chenyewe pamoja na kutokuwa na maktaba kwa aili ya kupata marejeo ya masomo.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.