Na Linus R. James
Hayo yamebainishwa mapema leo wakati kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya madawati katika shule ya Sekondari ya Ngh’ohoko iliyo Kata ya Ng’hohoko .
Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi Mwl. Mkuu wa shule ya Ng’hohoko alisema shule ina wanafunzi 268 ambapo kabla ya NMB ilikua na viti 406.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Bi Mwanaisham Nassor alisema kuwa hizi ni jitihada na maandalizi ya kuwapokea kidato cha tano mwakani.
“Kwanza usajili wa kidato cha kwanza mwakani tunategemea wawe wengi pili hili linaloendelea ni maandalizi ya kidato cha tano, niwashukuru wananchi wa Ng’hohoko kwa ushirikiano wa kuchangia elimu na ndio maana tumeichagua shule hii iwe mfano, miundo mbinu ipo ya kutosha ukiacha changamoto chache ambazo hazimzuii mwanafunzi kusoma au mwalimu kufundisha”
Naye diwani wa kata ya Ng’hoboko Mh Pius Machungwa akitoa salam kwa wananchi aliwapongeza sana wananchi kwa kuwa na ushirikiano wa kuchangia mambo mbali mbali hususani ujenzi wa miundombinu ya elimu ambapo alisema kuwa ameanzisha mkakati wa kila kaya kuchangia kiasi cha fedha za kitanzania 15,000 na tayari wamejenga nyumba nne.
“Niwapongeze wananchi wangu, tangu nilipopata udiwani mwaka 2000 niliwashawishi wananchi mwaka 2005 tukaienga shule hii na tukaijenga nab ado tunazidi kuongeza miundombinu ili shule yetu iwe ya mfano, serikali nayo inapenda kumsaidia mtu anayejishughulisha ivyo msichoke kuchangia maendeleo kwani uwezo wa kusimamia kila shilingi ninao na siana tamaa na shilingi ya mwananchi”
Aidha Mheshimiwa diwani huyo aliwasisitiza wananchi umuhimu wa kutunza fedha benki ambapo alisema mtu akiweka pesa benki kwanza anajiepusha na majanga na pili benki inapata mapato na ndiyo madawati wanayochangia.
Pia alimuomba Meneja wa benki ikiwezekana akasaidie pia katika ukamilisha wa majengo ya shule ya msingi Ng’hoboko ili wanafunzi waweze kuzalishwa kwa wingi vijjijini kwa ajili ya kujiunga n elimu ya sekondari.
Naye Mgeni Rasmi wa hafla hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Meatu Dr Joseph Chilongani wakati wa kuhutubia wananch na wanafunzi waliohudhuria i alisema kua aliwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii, kuwasihi wazazi na wadau wa maendeleo waendelee na moyo wa uchangiaji wa miundo mbinu hususani elimu na afya.
“Hiki wanachokifanya benki ya NMB ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, serikali inafanya mambo mengi makubwa ikiwemo kuleta fedha kila mwezi, ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu mbali mbali” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Pia aliwasistiza wazazi kulipa suala la mabweni kipaumbele kwani motto anapokua bweni au kwenye makambi ya elimu anapata muda wa kutosha kujisomea tofauti na anapkua nyumbai.
Akikabidhi madawati kwa niaba ya Benki ya NMB, Meneja wa kanda ya NMB Magharibi, Ndugu Sospeter Njile Magesse lisema madawati 50 yaani viti 50 na meza 50 yenye thamani ya shilingi milioni tano yametengenezwa hapa Wilayani Meatu ivyo licha ya kutoa madawati lakini fedha imebaki mikononi mwa wananchi wa Meatu.
Hafla hii fupi ilihudhuriwa na wananchi mbali mbali, wanafunzi, Kaimu Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mwanhuzi Bwana Dad Salim, Meneja wa kanda, Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri na Wakuu wa Idara na vitengo mbali mbali Diwani wa kata ya Ng’hoboko na viongozi wa kata hiyo iliongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dr. Joseph Chilongani.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.