"Hii ni timu yako ya ushindi, umetuamini hatutakuangusha." Anasema Waziri Bashungwa
OR- TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa (Mb) amesema wako tayari kuifia 'site' kuliko kumuangusha Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia Wananchi na kusimamia utekeleza miradi ya maendeleo.
Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo, mara baada ya kuapishwa kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ambao uteuzi wao umefanyika hivi karibuni, zoezi ambalo lilifanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam tarehe 01 Agosti 2022.
Waziri Bashungwa amesisitiza wizara yake kwenda kujipanga na kubadilika ili kuwa Wizara inayowahudumia Wananchi na kuwa Wizara inayotatua kero na changamoto za Wananchi kwa wakati.
Alisema asilimia 70 ya Watumishi wa umma wako Ofisi ya Rais -TAMISEMI na kuwa kila mmoja akitekeleza wajibu wake ina maana utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi itatekelezwa kwa zaidi ya asilimia 70.
Bashungwa alisema kwa mwaka wa fedha 2021/22, Ofisi ya Rais - TAMISEMI imeweza ukusanyaji mapato na kuvuka malengo kwa kukusanya asilimia 103 na kusisitiza kuwa bado kuna fursa kubwa ya kuongeza malengo haya.
" Mheshimiwa Rais umetuelekeza tuhakikishe tunadhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato, timu hii iliyopo mbele yako mara baada ya kuapa, tunakwenda kujipanga na tunataka dhamira yako (Rais Samia) ya kuwahudumia wananchi kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI ikatimie, tuko tayari kufia site kuliko kukuangusha." Amesema Waziri Bashungwa.
Aidha, Bashungwa alimuahidi Rais kuwa timu hiyo wataekenda kutekeleza maagizo anayoyato ikiwamo ya ukusanyaji mapato na kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za miradi.
"Nikuhakikishie Mheshimwa Rais hii ndio timu yako ya ushindi, umetuamini hatutakuangusha." Amesema Bashungwa.
Pia, aliwakumbusha Wakuu wa Mikoa kujipanga kuhakikisha Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23, 2022 inafanyika kwa mafanikio.
Matukio katika Picha
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.