Tuzo hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji lililofanyika Mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa Mtaka amesema kuwa Tuzo hizi ni hamasa kwa Viongozi na wananchi wa Simiyu kuongeza jitihada zaidi katika utekelezaji wa Sera ya Viwanda kuelekea kwenye Uchumi wa kati.
Mkoa wa Simiyu unatekeleza Sera ya Viwanda chini ya Kauli Mbiu ya “WILAYA MOJA BIDHAA MOJA” na hadi sasa kuna kiwanda cha kutengeneza Chaki kilichopo wilayani Maswa na Kiwanda cha kusindika Maziwa wilayani Meatu, ambapo upembuzi yakinifu unaendelea kwa ajili ya upanuzi wa viwanda hivi ili kuongeza uzalishaji.
Aidha, upembuzi yakinifu utafanyika katika Halmashauri nyingine kwa ajili ya kuanzisha viwanda mbalimbali kikiwemo kiwanda cha sabuni za maji, za unga na mche wilayani Itilima, Kiwanda cha kutengeneza Tomato Sauce na Chill Sauce Wilayani Busega na kiwanda cha kusaga nafaka na kupaki unga Bariadi Mjini.
Vingine ni kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi kitakachojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Kiwanda cha kutengeneza vifungashio kitakachojengwa Wilayani Maswa.
Pamoja na viwanda hivyo, Mkoa umekusudia kujenga Kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba ambacho kitasaidia Taifa kuokoa fedha zilizokuwa zikitumika kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.