Na Linus R. James ( Meatu DC)
Shirika la AMREF( Tanzania na Canada) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Marie Stopes International, Deloitte na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wameendelea kuboresha huduma ya afya kwa jamii hususani wazazi kupitia wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Hayo yamebainishwa mapema leo wakati wa makabidhiano ya baiskeli 69 zenye jumla thamani ya shilingi 16, 524,000 za Kitanzania yaliyofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Meatu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Afisa Mradi Uzazi na Uzima Ndg. Henericko Ernest alisema lengo la mradi wa uzazi na uzima ni kuzidi kushirikiana na Wilaya ya Meatu pamoja na wadau wa afya kuhakikisha wanapunguza vifo.
“ Mwaka jana Mwezi wa saba na wa nane tulitoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya vijiji kwa ajili ya kuhamasisha wazazi kuhudhuria kliniki na vituo vya afya pamoja na masuala ya lishe na leo tunakabidhi baiskeli hizi ili yale waliyoyapata katika mafunzo yaweze kufanyiwa utekelezaji kikamilifu ” Alisema Ndg. Henericko.
Afisa mradi huyo alisema kuwa mbali na kutoa mafunzo walihahidi kusaidia vitendea kazi mbali mbali, vikiwemo baiskeli, maboresho ya huduma za dharula yaani wodi ya wazazi na upasuaji, pamoja na kuboresha miundombinu ya maji katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Naye Kaimu Mganga mkuu wa hospitali ya Wilaya Dr. Frank Mganga akitoa shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa baikeli hizi zitaleta chachu
“Hizi Baiskeli 69 Kituo cha afya Mwandoya kitapata baiskeli 40, Zahanati ya Ng’hoboko 16 na Imalaseko 13, baiskeli hizi zimezingatia idadi ya wahudumu waliopo katika vituo husika katika ngazi ya afya ivyo naamini zitaleta chachu katika kuboresha na kuimarisha huduma ya afya kwa wananchi ndani ya Wilaya ya Meatu” Alisema Dr. Mganga.
Aidha baada ya makabidhiano katika halmashauri ya wilaya baiskeli hizo zmesambazwa kwenye vituo husika na zitakua chini ya usimamizi wa vituo husika, uongozi wa kijiji chini ya ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya.
Ikumbukwe kuwa mradi wa Afya na uzima unatekelezwa katika mkoa wa Simiyu kwa kipindi cha miaka miine katika Wilaya zote za Simiyu ambapo ulianza mwaka 2017 na unatarajia kukamilika mwaka 2020.
MWISHO
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.