Ili uweze kupata kitambulisho cha Taifa (kitambulisho cha uraia) kwanza unatakiwa ujaze fomu maalum ya maombi ya kitambulisho cha Taifa ambayo utaipeleka kwenye ofisi ya serikali ya mtaa/kitongoji unapoishi kwa ajili ya kuweka saini na muhuri.
Baada ya hapo utaipeleka fomu yako kwenye ofisi za NIDA zilizopo wilayani kwako kwa ajili ya usajili na uchukuaji wa alama za kibaiolojia.
Kumbuka kuambatanisha fomu yako iliyojazwa kikamilifu na yenye muhuri pamoja na vivuli vya nyaraka ulizonazo kati ya nyaraka zifuatazo: cheti cha kuzaliwa, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi, kadi ya kupigia kura, leseni ya udereva, Utambulisho wa mlipa kodi (TIN Number), pocha ya pasipoti (Passport size), cheti cha kidato cha 4 na 6, kadi ya bima ya afya, kadi ya uanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii.
Kwa maelezo zaidi na kupata fomu tembelea ofisi za NIDA zilizopo katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.