• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Meatu District Council
Meatu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Halmashauri ya Wilaya ya Meatu

  • Mwanzo
    • sub home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Core Values
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Miundombinu, Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Pre Primary Education
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango na Uratibu
      • Utumishi, Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Maliasili na Utunzaji wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha
      • Uratibu wa Manunuzi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji na Uvuvi
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Fishing
    • Expertise
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao
      • Fedha, Uongozi na Mipango
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha habari

Waziri Jafo awasilisha makadirio ya bajeti 2020/2021

Imewekwa: April 8th, 2020

Kutoka OR- TTAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameliomba bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha kiasi cha shilingi Trioni 7.02 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Akiwasilisha hoja hiyo Bungeni leo Jijini Dodoma Mhe Jafo amesema  makadirio hayo  yanahusisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-(OR-TAMISEMI), Tume ya Utumishi wa waalimu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akifafanua zaidi Mhe Jafo amesema kiasi cha shilingi Trilioni 3.8  kitatumika  kwa ajili ya mishahara, Bilioni 851 kwa matumizi mengine na kiasi cha shilingi trilioni 2.29 kitatumika  kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 Serikali imepanga kusimamia utawala bora, kukuza demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi na Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma (D by D)

Ameendelea  kufafanua kuwa Serikali itaendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za utoaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari  katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa ikijumuisha utekelezaji wa mpango wa utoaji wa Elimumsingi Bila Ada

Akifafanua zaidi Mhe.Jafo amesema Serikali inampango wa kuratibu ujenzi wa miundombinu ya maeneo ya utawala katika Mikoa, Wilaya, na Halmashauri mpya na za zamani zipatazo 30 ambazo zinatakiwa  kuhamia katika maeneo yao ya Utawala

Kuhusu ujenzi wa  majengo ya utawala na nyumba za viongozi amesema Serikali itaendelea na ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa majengo ya Ofisi na nyumba za makazi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Makatibu Tawala Wasaidizi, Maafisa Tarafa na watumishi waandamizi

Hata hivyo amesema itafanya matengenezo ya barabara zenye urefu wa Kilometa  23,175.11,  Makaravati2, 052 na mifereji ya maji ya mvua  yenye urefu wa 79.9, Ujenzi wa Madaraja 80  yaliyopo  vijijini na mijini ili kuimarisha miundombinu ya barabara nchini .

Kwa upande wa Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara Mhe. Jafo amesema Serikali itajenga barabara zenye urefu wa kilometa 35.3 kwa kiwango cha lami na ukarabati urefu wa kilometa 321 kwa kiwango cha changarawe , kukamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 47.59 kwa kiwango cha lami Jiji la Dar-es-salaam.

Wakati Huohuo Mhe. Jafo amesema Serikali itaanza  ujenzi wa barabara ya Nzasa-Kilungule-Buza,Ulongoni-Bangulo-Kinyerezi  na Magomeni Mapipa- Urafiki na ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 11.7 kwa kiwango cha lami katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni

Mhe. Jafo amesema katika suala la afya Seikali  itaendelea kujenga miundombinu ya afya  ambapo  kutajengwa  wodi tatu  katika kila Hospitali ya Halmashauri, kuendelea na ujenzi wa  Hospitali  27, ujenzi wa Zahanati 3 katika kila Halmashauri na ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali 67 zilizojengwa.

Aidha  Mhe. Jafo  amesema katika mwaka wa Fedha wa 2020/2021 Serikali imepanga  kutumia shilingi bilioni 42.3 kwa ajili ya ujenzi wa maabara za sekondari ambazo zitajengwa katika kila Halmashauri.

MWISHO

Chanzo 

OR TAMISEMI

Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi September 16, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji kwa Ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa September 16, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 20, 2024
  • Taarifa ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Matokeo ya Mwanzo February 20, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi Karibuni

  • Jamii Yatakiwa Kupinga Mila Potofu, Kandamizi

    March 08, 2023
  • Meatu Pikipiki Tisa

    February 14, 2023
  • TAKUKURU RAFIKI

    January 27, 2023
  • Hongereni Wataalam: Ngatumbura

    January 27, 2023
  • Angalia zote

Video

Ziara ya Waheshimiwa mawaziri nane Wilaya ya Meatu kwa ajili ya kukusanya Maoni ya Kutatua Migogoro
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Miongozo Mbali mbali
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari
  • Dokumenti mbali mbali

Tovuti mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara ya Takwimu(NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu huria
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Meatu, Simiyu, Tanzania

    Anwani ya Posta: S.L.P 44

    Simu: 028 2795 008

    Simu ya Mkononi: 0622 404 712

    Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.