Shirika la Mendeleo la Uingereza (DFID) kupitia Mpango wa Kuboresha Elimu Tanzania (EQUIP-T) limetoa jumla ya shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya Elimu katika Halmashauri zote za mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vyerehani 50 kutoka Ubalozi wa China, kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Nkoma Itilima, Makabidhiano ya. Hundi ya Shilingi Milioni 178 kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo zilizotolewa na Balozi wa China, na uwasilishwaji wa Taarifa za mashirika wadau wa Maendeleo mkoani Simiyu (DFID, AMREF na UNFPA), ambayo ilishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Mtaka amesema fedha hizo zimeshapokelewa katika Akaunti za Halmashauri zote za Mkoa huo na wiki ya kuanzia tarehe 26 Februari, 2018 Halmashauri hizo zitaanza kujenga miundombinu ya Elimu.
Mtaka ametoa shukrani zake kwa Shirika hilo ambalo amesema limechangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko katika Elimu na kuufanya mkoa wa Simiyu kutoka kwenye nafasi za mwisho kwenye ufaulu hadi kufikia nafasi ya 11 kwa mwaka 2017. Read more......
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.