• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Meatu District Council
Meatu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Halmashauri ya Wilaya ya Meatu

  • Mwanzo
    • sub home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Core Values
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Miundombinu, Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Pre Primary Education
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango na Uratibu
      • Utumishi, Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Maliasili na Utunzaji wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha
      • Uratibu wa Manunuzi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji na Uvuvi
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Fishing
    • Expertise
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao
      • Fedha, Uongozi na Mipango
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha habari

Serikali imefuta tozo za mazao ya Chai, Pamba na Kahawa

Imewekwa: April 15th, 2017

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefuta baadhi ya tozo katika mazao ya pamba, chai na kahawa ambazo ni kero kwa wakulima ikiwemo ya sh. 450,000 iliyokuwa inatolewa na kila kiwanda cha kuchambua pamba kwa ajili ya kuchangia mbio za Mwenge.

Amesema tozo nyingine iliyofutwa kwa zao la pamba ni ada ya vikao vya Halmashauri za Wilaya ambayo ni sh. 250,000, ambapo katika zao la chai kodi ya moto na uokoaji imeondolewa na kwenye zao la kahawa, ada ya leseni ya kusindika kahawa ya Dola za Marekani 250 imefutwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 6, 2017) wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2017/2018 Bungeni mjini Dodoma.

Amesema kufutwa kwa tozo hizo ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali kwa wakulima nchini ili kuwapunguza kodi, tozo na ada mbalimbali zinazochangia kuwapunguzia faida.

“Serikali pia imeboresha mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuanzisha utaratibu wa wazi wa ununuzi wa mazao kupitia minada. Na katika msimu wa mwaka 2016/2017 kwenye zao la korosho, utaratibu huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa bei ya korosho kwa kilo kutoka sh.  1,200 hadi sh. 3,800, bei ambayo haijawahi kufikiwa katika historia ya zao la korosho nchini,” amesema na kushangiliwa.

Amesema mfumo huo wa stakabadhi ghalani na utaratibu wa minada umeongeza ushindani na kuvutia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi hususan nchi ya Vietnam na nchi nyingine kuja wenyewe kununua korosho badala ya kutegemea soko la India pekee.

Waziri Mkuu amesema katika mwaka 2017/2018, Serikali itaendelea na uchambuzi wa kina wa kodi, tozo na ada zilizobaki katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kwa lengo la kuziondoa au kuzipunguza ili kumwezesha mkulima kunufaika zaidi na jasho lake na kuongeza mapato ya Halmashauri.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Bunge lilipitisha Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016, ambayo ni muhimu katika kuimarisha usimamizi na uwajibikaji katika sekta ya habari nchini, ambapo kanuni za sheria hiyo zimeandaliwa na tayari zimeanza kutumika.

“Natoa wito kwa wadau wa sekta ya habari kuzingatia sheria na kanuni hizo ili kuimarisha weledi katika tasnia ya habari. Ninashauri wajikite zaidi katika kuandika na kutangaza habari za masuala ya maendeleo na uchumi ili kuwasaidia wananchi kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha huduma za kijamii,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amevikumbusha vituo vya televisheni kuweka wakalimani wa lugha kwenye vituo vyao. Amesema katika mwaka 2017/2018, Serikali itaendelea kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu shuleni na vifaa vya kufundishia.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwamba Serikali imeendelea kutoa huduma pamoja na kuongeza upatikanaji wa haki na fursa kwa watu wenye ulemavu na katika kutimiza azma hiyo, amewaagiza Wakuu wa Mikoa wahakikishe kuwa Kamati za Watu wenye Ulemavu zinaanzishwa katika ngazi za Mikoa, Wilaya, Mitaa na Vijiji.

Amesema Serikali pia imeanzisha kampeni za kupinga unyanyapaa na vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino katika mikoa 11 ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu, Kagera, Tabora, Kigoma, Mara, Mbeya, Katavi na Rukwa na kwamba kampeni hiyo itaendelea nchi nzima.

Chanzo: www.pmo.go.tz


Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi September 16, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji kwa Ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa September 16, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 20, 2024
  • Taarifa ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Matokeo ya Mwanzo February 20, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi Karibuni

  • Jamii Yatakiwa Kupinga Mila Potofu, Kandamizi

    March 08, 2023
  • Meatu Pikipiki Tisa

    February 14, 2023
  • TAKUKURU RAFIKI

    January 27, 2023
  • Hongereni Wataalam: Ngatumbura

    January 27, 2023
  • Angalia zote

Video

Ziara ya Waheshimiwa mawaziri nane Wilaya ya Meatu kwa ajili ya kukusanya Maoni ya Kutatua Migogoro
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Miongozo Mbali mbali
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari
  • Dokumenti mbali mbali

Tovuti mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara ya Takwimu(NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu huria
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Meatu, Simiyu, Tanzania

    Anwani ya Posta: S.L.P 44

    Simu: 028 2795 008

    Simu ya Mkononi: 0622 404 712

    Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.