Mgombea wa Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndg. Nawida J. Nawida ameshinda na kuwa Diwani wa kata ya Mwanhuzi baada ya kuwabwaga wenzake katika uchaguzi mdogo uliofanyika Ktika kata ya Mwanyahina wilaya ya Meatu jana.
Akitangaza matokea ya uchaguzi, mwenyekiti wa Uchaguzi wilaya ya Meatu ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Meatu Ndg Fabian Manoza Said amesema
“Diwani tutakayemtangaza leoambaye ndio mshindi, tutamkabidhi cheti leo, lakini keshokutwa jumatatu, tutamuapisha, tutamuapisha Jumatatu kwa sababukata ya MwanyahinaWDC yake ilikua haifanyi kazi, kwa hiyo tukisha muapisha Mh Diwani anatakiwa akakae na WDC yake kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ili watoto wetu tarehe 15 mwezi wa pili wajiunge namasomo ya kidato cha kwanza”
Akitoa utanguliziNdg Manoza alisema mchakato wa uchaguzi ulianza tarehe 21 kwa wagombea kuchukua fomu ambapo tarehe 27 waliteuliwa nakampeni zilianza tarehe hiyo.
Aidha Mwenyekiti huyo alibainisha changamoto ya mvua ambazo ziliwakumba wasimamizi pamoja na wapiga kura Wakati wa kupeleka vifaa kwenye vituo vya kupigia kura, wakati wananchi wanajitokeza kupiga kura na wakati wa kurudisha vifaa na matokeo.
“Matokeao ya ujumla yameathirika kwa sababu baadhi ya wananchi wameshindwa kufika kwa sababu ya mvua kubwa iliyonyesha kuanzia jana na leo” Alisisitiza Manoza
Aidha watu kati ya 4859 walioandikishwa, 1940 walijitokeza kupiga kura kati ya hao kura 11 ziliharibika na matokeo yalikua kama ivi: Ndg N.J. Nawida wa CCM alipata jumla ya kura 1684 sawa na 87.30%, Ndg. S.Y Magida wa ACT alipata jumla ya kura 139 sawa na 7.21%, Ndg. N.A Anatory wa CHAUMA alipata jumla ya kura 59 sawa na 3.06% na Ndg. S.M. Edward wa TLP alipata jumla ya kura 47 sawa na 2.44%.
Kwa matokeo hayo yamemfanya Ndg Nawida J. Nawida kuiongoza kata ya Mwanyahina kupitia chama cha Mapinduzi.
Mwisho
Matokeo zaidi kwa vituo
|
KITUO | ACT | CCM | CHAUMA | TLP | JUMLA |
1 | OFISI YA VEO MWAGWILA-1 | 15 | 229 | 4 | 1 | 249 |
2 | OFISI YA VEO MWAGWILA-2 | 6 | 247 | 5 | 1 | 259 |
3 | OFISI YA VEO MWANYAHINA -1 | 0 | 217 | 0 | 0 | 217 |
4 | OFISI YA VEO MWANYAHINA -2 | 7 | 61 | 1 | 0 | 69 |
5 | S/AWALI MWAMSINGI – 1 | 3 | 28 | 2 | 0 | 33 |
6 | S/AWALI MWAMSINGI – 2 | 4 | 155 | 5 | 6 | 170 |
7 | S/M BUSIA – 2 | 0 | 200 | 0 | 7 | 207 |
8 | S/M BUSIA – 1 | 2 | 80 | 0 | 0 | 82 |
9 | S/M MWAJIDALALA – 1 | 22 | 45 | 1 | 0 | 68 |
10 | S/M MWAJIDALALA – 2 | 38 | 120 | 8 | 5 | 171 |
11 | S/M MWANYAHINA -2 | 5 | 40 | 0 | 0 | 45 |
12 | S/M MWANYAHINA – 1 | 3 | 52 | 0 | 0 | 55 |
13 | S/M MWAGWILA -1 | 4 | 39 | 1 | 0 | 44 |
14 | S/M MWAGWILA -2 | 30 | 171 | 32 | 27 | 260 |
|
JUMLA | 139 | 1684 | 59 | 47 | 1929 |
|
ASILIMIA | 7.21% | 87.30% | 3.06% | 2.44% |
|
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.