Na Linus R. James - MEATU DC
Halmashauri yawilaya ya Meatu kupitia Idara ya maendeleo ya jamii, idara ya maji, mazingira, mifugo na uvuvi imekiwezesha kikundi cha akina mama cha Ngunani kilichopo kijiji cha Jinamo kata ya Mwanjolo ili kiweze kujiinua kiuchumi.
Katika uwezeshwaji huo leo Idara hizo nne zimeweza kutoa mafunzo ya namna bora ya ufugaji wa samaki aina ya Sato lengo likiwa ni kutaka kikundi hicho kufuga ufugaji wa kisasa na wenye tija.
Licha ya kutoa mafunzo halmashauri kupitia asilimia nne ya mapato ya ndani kwenye mfuko wa maendeleo kwa wanawake(WDF) imeweza kutoa kiasi cha shilingi milioni nane kwa kikundi hicho cha Ngunani.
Jumla ya vifaranga vipatavyo 11, 000 vimepandikizwa katika bwawa la Jinamo lililopo katika kata ya Mwanjolo.
Akizungumza wakati akitoa mafunzo Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Mwanaisham Nassor amesema hii ni fursa ya kuwainua akina mama kiuchumi kama mbinu zilizotoloewa na wataalam wote zitazingatiwa na kufuatwa
“Jumla ya vifaranga 11,000 ambavyo tumeshavipandikiza tunategemea ifikapo mwezi wa sita mwaka huu kikukndi hiki kitaweza kuvuna samaki wasiopungua 10,000 ivyo kujipatia fedha za Kitanzania zisizopungua milioni thelasini ivo kipato na uchumi wa wanakikundi vitaongezeka”. Alisema Bi Mwanaisham.
Mafunzo haya ya vikundi ni mwendelezo wa Halmashauri kupitia Idara ya maendeleo ya Jamii kuyafikia makundi mbali mbali wakiwemo Wanawake, vijana na watoto ambapo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 jumla ya vikundi visivyopungua 70 vimepangwa kufikiwa na kuwezeshwa.
Mwisho
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.