Na Linus R. James - Meatu DC
Halmashauri za Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu na Iramba Mkoani Singida zimekubaliana kwa pamoja kuwa na mikakati ya kuboresha na kutunza mazalia ya samaki katika Ziwa Kitangiri ikiwa ni pamoja kufunga ziwa Kitangiri yaani mkakati wa mda mfupi pamoja na kutengeneza sheria ndogo ndogo na Miongozo ambayo itakakua ni mikakati ya mda mrefu.
Makubaliano hayo yamefanyika jana katika kikao cha pamoja cha ujirani mwema kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Meatu Mkoani Simiyu kikihusisha kamati za ulinzi na usalama, Waheshimiwa madiwani, Wenyekiti wa Halmashauri, Viongozi wa Chama cha Mainduzi , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Fabian Manoza Said pamoja na wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri zote mbili.
Akifungua kikao hicho cha Ujirani mwema Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dk. Joseph Chilongani alisema
‘’ Ni jukumu letu sisi viongozi wa Wilaya hizi kuhakikisha tunatunza na kuhifadhi mazingira ya Ziwa Kitangiri ili kutoa fursa samaki wazaliane kwa wingi na wakubwa kwa ajili ya kitoweo kwa jamii na kuwaongezea kipato wananchi kwa ujumla pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri zetu.’’
‘’ Cha msingi Halmashauri wilaya za Iramba Meatu, Igunga na Wilaya ya Kishapu tulikuwa na utaratibu wa pamoja za Kufunga Ziwa Kitangiri kila mwaka lakini hatukuwa mpango mkakati wa pamoja kuamua ni lini ziwa hili litakuwa linafungwa kila mwaka, hata hivyo katika kikao cha Ujirani mwema tuliofanya mjini Shinyanga mwaka juzi tulikubaliana kuhifadhi Ziwa Kitangiri na kupiga vita kwa nguvu uvuvi haramu na kuhakikisha mazingira ya Ziwa yanakua mazuri ili samaki wazaliane kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.’’ Alisisitiza Dkt. Chilongani
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula alisema tayari kwa upande wa Wilaya ya Iramba Ziwa Kitangiri limeshafungwa toka tarehe 01 mwezi Januari na litafunguliwa tarehe 01 mwezi Aprili 2019
‘’ Ndugu Mkuu wa Wilaya ya Meatu kwa upande wetu tulikwisha funga Ziwa Kitangiri kama kawaida yetu ya kila mwaka isipokuwa mwaka huu tumeona tuje kujiriridhisha katika Wilaya ya Meatu maana miaka yote sisi tulikuwa tukifunga Ziwa upande wa Meatu wanavua hii ilikuwa inawatia unyonge sana wavuvi wa upande wa Iramba’’
Wakiwa katika Kijiji cha Usulize Wilayani Meatu kwenye kambi ya wavuvi ya kijiji hicho Mheshimiwa mkuu wa Wilaya alitangaza rasmi kufunga Ziwa hilo kwa uande wa Meatu.
‘’ Mkuu wa Wilaya ya Iramba na Wenyeviti wa Halmshauri zote na kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya hizi leo hii natamka kuwa Ziwa Kitangiri limefungwa hadi tarehe 01 mwezi Aprili mwaka huu hivyo kuanzia tarehe 17/04/2019 ndiyo Ziwa litafunguliwa Rasmi na shughuli za uvuvi zitaanza tena na yeyote atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria’’ alionya Mkuu huyo wa Wilaya.
Kikao hicho cha ujirani mwema kimewaeleza wataalamu wa Halmashauri za Wilaya za Meatu, Iramba, Kishapu na Igunga ambao wananchi wake wanaonufaika na Ziwa hilo watengeneze Rasimu na kuweka sheria ndogo ndogo za kulinda Ziwa hilo na wamepewa mwezi mmoja kuandaa rasimu hiyo ambayo itakuwa ndiyo dira ya kudhibiti Ziwa hilo lisihujumiwe
MWISHO.
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.