Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt.Joseph Chilongani pamoja na wataalam wa Halmashauri ya Meatu kutunga sheria ndogo zitakazosaidia kulinda na kutunza bwawa la maji la Mwanjoro.
Mhe. Makamu wa Rais amesema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mwanjoro mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa bwawa la maji la Mwanjoro lililopo kata ya Mwanjoro Wilayani humo.
Mhe.Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua uwepo wa tatizo la maji na ukame uliopo Wilayani Meatu ndiyo maana imeamua kujenga bwawa hilo litakalogharimu shilingi bilioni1.3 kwa awamu ya kwanza, hivyo ni lazima kuwepo na sheria ndogo zitakazosaidia kufanya bwawa hilo lidumu na kutoa huduma endelevu kwa wananchi. Soma zaidi...
Meatu, Simiyu, Tanzania
Anwani ya Posta: S.L.P 44
Simu: 028 2795 008
Simu ya Mkononi: 0622 404 712
Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.