• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Meatu District Council
Meatu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Halmashauri ya Wilaya ya Meatu

  • Mwanzo
    • sub home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Core Values
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Miundombinu, Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Pre Primary Education
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango na Uratibu
      • Utumishi, Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Maliasili na Utunzaji wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha
      • Uratibu wa Manunuzi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji na Uvuvi
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Fishing
    • Expertise
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao
      • Fedha, Uongozi na Mipango
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha habari

JPM atoa salamu za pole kwa majeruhi wa ajali Simiyu

Imewekwa: September 10th, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa pole kwa waandishi wa habari watano wa Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani waliopata ajali katika wilayani Meatu, wakati akiwa ziarani wilayani humo, salamu ambazo zimewasilishwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, ambaye aliwatembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu walikokuwa wakipatiwa matibabu.

Akiwasilisha salamu za Mhe.Rais,  Mhe. Mtaka amesema magari matano ya Simiyu ya Serikali na gari binafsi yaligongana na watu sita wakajeruhiwa wakiwemo waandishi watano na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani  na kusisitiza kuwa Mhe. Rais ameguswa na jambo hilo, hivyo ametoa shilingi laki tano kwa kila majeruhi ili iwasaidie katika matibabu.

“...magari ya waandishi wa habari lakini kulikuwa na gari binafsi, baada ya msafara wa Rais kwa sababu ya vumbi,  dereva mmoja katika yale magari alisimama kutaka kuona njia vizuri, magari yaliyokuwa yakifuatana  matano yakagongana kwa nyuma, watu sita wakapata majeraha miongoni mwao walikuwepo waandishi wetu watano na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani”

“Mhe. Rais anatoa salamu zake za pole kwa majeruhi wote,  ameguswa sana na jambo hili hasa pale aliposikia kuwa sehemu ya majeruhi ni waandishi ambao tumekuwa nao pamoja katika ziara hii, wakafanya kazi kubwa ya kuuhabarisha Watanzania,  akaomba mimi kama Mkuu wa Mkoa nifikishe salamu zake za pole kwa niaba  yake kwa watu hawa sita” alisema.

Ameongeza kuwa Mkoa utaendelea kuchukua tahadhari kupitia jeshi la polisi hasa katika misafara ya viongozi na kuhakikisha kuwa wanajenga uelewa wa pamoja kwa madereva wakati wa maandalizi ya safari juu ya namna ya kuchukua tahadhari

.Rehema Evance ambaye ni mwandishi wa Azam TV amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatambua na kuona awape mkono wa pole ambao amebainisha kuwa fedha hizo zitawasaidia katika kugharamia matibabu.

“ Kwanza namshukuru Mungu kwa kutujalia tukapona,  lakini kipekee napenda kumshukuru Mhe. Rais kwa kuona kuna haja ya kutusaidia katika hili, kwa hiki alichotoa Mungu ambariki sana kitatusaidia kwenye matibabu, tunaahidi kuendelea kuwahabarisha Watanzania na kuhakikisha yale yote yanayotendeka ndani ya nchi yanawafikia” alisema.

Ajali hii iliyotokea wilayani Meatu Septemba 09, 2018 imesababisha majeruhi sita ambao ni waandishi watano Rehema Evance (AZAM TV), Belensi China(ITV), Aidan Mhando(Channel Ten), Phaustine Fabian(Mwananchi), Mpiga Picha Samson Masunga pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani na hakuna kifo kilichotokea..

Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Hospitaliya Wilaya ya Meatu ambapo waandishi wa habari Rehema Evance (AZAM TV), Phaustine Fabian(Mwananchi), Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani waliruhusiwa na Belensi China(ITV), Aidan Mhando(Channel Ten), na Mpiga Picha Samson Masunga walipewa Rufaa kwenda Bugando kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Matangazo

  • Tangazo la Nafasi za Kazi September 16, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji kwa Ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa September 16, 2024
  • Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 February 20, 2024
  • Taarifa ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Matokeo ya Mwanzo February 20, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi Karibuni

  • Jamii Yatakiwa Kupinga Mila Potofu, Kandamizi

    March 08, 2023
  • Meatu Pikipiki Tisa

    February 14, 2023
  • TAKUKURU RAFIKI

    January 27, 2023
  • Hongereni Wataalam: Ngatumbura

    January 27, 2023
  • Angalia zote

Video

Ziara ya Waheshimiwa mawaziri nane Wilaya ya Meatu kwa ajili ya kukusanya Maoni ya Kutatua Migogoro
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Miongozo Mbali mbali
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari
  • Dokumenti mbali mbali

Tovuti mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara ya Takwimu(NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu huria
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Meatu, Simiyu, Tanzania

    Anwani ya Posta: S.L.P 44

    Simu: 028 2795 008

    Simu ya Mkononi: 0622 404 712

    Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.