• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Meatu District Council
Meatu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Halmashauri ya Wilaya ya Meatu

  • Mwanzo
    • sub home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Core Values
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Miundombinu, Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Pre Primary Education
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango na Uratibu
      • Utumishi, Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Maliasili na Utunzaji wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha
      • Uratibu wa Manunuzi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji na Uvuvi
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Fishing
    • Expertise
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao
      • Fedha, Uongozi na Mipango
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha habari

Ninawezaje kuanzisha Biashara?

Kuanzisha Biashara

Katika ukurasa huu utaona viungo vitakavyokuongoza kuhusu mambo ya msingi unayohitaji kufanya wakati unapoanzisha biashara kama mtu binafsi, ubia, amana au kampuni yenye dhima ya ukomo. Pia utaona viungo vinavyokuelekeza kwenye msaada zaidi na huduma zinazotolewa na TRA kwa mashirika mapya ya biashara.

 

Unatakiwa kufanya nini unapotaka kuanzisha biashara?

Mtu Binafsi

Mtu binafsi awe mkazi au si mkazi anatakiwa kutembelea ofisi ya TRA ya mkoa au wilaya na kujaza fomu ya maombi ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN). Maombi yanaweza kufanywa pia kwa njia ya mtandao, hata hivyo mwombaji lazima afike ofisi za TRA kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole pamoja na kupiga picha na kuweka saini.

 

Baada ya kupata cheti cha namba ya utambulisho wa mlipakodi mwombaji atatakiwa kuomba leseni ya biashara kutoka ofisi za Biashara katika Wilaya, Manispaa, Jiji na Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kutegemea aina ya biashara anayotaka kuanzisha.


Mkazi ni Nani?

Mtu anastahili kuwa mkazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa:-

  • Atakuwa na makazi ya kudumu katika Jamhuri ya Muungano na atakuwepo wakati wowote katika kipindi cha mwaka wa mapato.
  • Yupo katika Jamhuri ya Muungano katika mwaka wa mapato kwa kipindi au vipindi vinavyofikisha jumla ya siku 183 au zaidi.
  • Yupo katika Jamhuri ya Muungano katika mwaka wa mapato na kila moja ya miaka miwili iliyotangulia ya mapato kwa vipindi vinavyofikia wastani wa siku 122 katika kila moja ya mwaka huo wa mapato.
  • Ni mwajiriwa au ofisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano aliyepangiwa kazi nje ya nchi katika mwaka wa mapato.

 

Hati ya Usajili:

Mtu binafsi anaweza kuamua kusajili jina la biashara kwa wakala aliyepewa kazi hiyo na Wizara ya Biashara na Viwanda anayejulikana kama Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Jina lililosajiliwa linaweza kupatikana kabla au baada ya kutoa maombi ya TIN. Jina la biashara lililosajiliwa litaonyeshwa kwenye hati ya TIN pamoja na jina la mtu huyo ikionyesha jina la mmiliki wa biashara kama (T/A).

 

Shirika (kampuni yenye dhima ya ukomo)

Kuanzisha shirika kunahitaji mtu aombe kupatiwa Hati ya shirika kutoka Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Wahamasishaji wa kampuni wanatakiwa kuandaa na kuwasilisha hati  na Mkataba na kanuni za kampuni.

Hati ya usajili wa shirika iambatishwe kwenye maombi ya TIN pamoja na Mkataba na Kanuni za Kampuni wakati mtu anapopeleka maombi TRA.

Kampuni yenye dhima ya ukomo itaomba kupatiwa hati ya TIN kwa kujaza fomu za maombi kama ifuatavyo:

  • Maombi kwa ajili ya kampuni.
  • Maombi kwa ajili ya wanahisa/wakurugenzi, iwapo mkurugenzi yeyote kati yao ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine anaweza kutoa maombi mengine. Namba ileile ya TIN itatumika.
  • Kwa wakurugenzi ambao si raia wanapaswa kutimiza masharti yote ya uhamiaji na kupata kibali cha biashara kutoka Idara ya Uhamiaji inayofanya kazi chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

 

     Ubia

Wabia wanatakiwa kusajili kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonyesha namba na majina ya wabia pamoja na mgawanyo wa hisa zao. 

  • Katika kutoa maombi ya TIN kampuni ya ubia itaomba kupatiwa hati kwa kuwasilisha nakala ya usajili waliyopata BRELA.
  • Kila mbia ataomba kupatiwa TIN, iwapo mbia yeyote tayari ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine hatakiwi kutoa maombi mengine. Namba ileile ya TIN itatumika.

 

 Udhamini

Udhamini ni mpango ambapo wadhamini wanamiliki mali lakini haihusishi ubia na kampuni.

 

Amana inapaswa kusajiliwa kama kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonesha majina na anwani za wadhamini. Kila mdhamini anapaswa kuomba kupatiwa hati ya TIN, iwapo mdhamini yeyote kati yao akiwa ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine hawezi kutuma maombi mengine. Namba ya TIN aliyo nayo itatumika.

 

Shirika la msaada:

Shirika hili litatambulika kama shirika la msaada kwa madhumuni ya masuala ya kodi baada ya kupatiwa kibali na Kamishna Mkuu. Mwombaji anatakiwa kupata nyaraka zote muhimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.

Tamko la Makadirio ya Mapato

Utatakiwa kutoa tamko la makadirio ya mapato kwa ajili ya kufanyiwa makadirio  ya awali ya kodi kwa mwaka husika. Afisa wa kodi anaweza kukuhoji na kurekodi taarifa za biashara yako na taarifa zako binafsi katika ofisi ya TRA.

Chanzo: Mamlaka ya Mapato Tanzania


Matangazo

  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Mwaka 2023 December 14, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba (PSLE) 2022 December 01, 2022
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani November 30, 2022
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Zoezi la Kitaifa la Chanjo ya Polio Awamu ya Nne November 30, 2022
  • Angalia zote

Habari za hivi Karibuni

  • Jamii Yatakiwa Kupinga Mila Potofu, Kandamizi

    March 08, 2023
  • Meatu Pikipiki Tisa

    February 14, 2023
  • TAKUKURU RAFIKI

    January 27, 2023
  • Hongereni Wataalam: Ngatumbura

    January 27, 2023
  • Angalia zote

Video

Ziara ya Waheshimiwa mawaziri nane Wilaya ya Meatu kwa ajili ya kukusanya Maoni ya Kutatua Migogoro
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Miongozo Mbali mbali
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari
  • Dokumenti mbali mbali

Tovuti mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara ya Takwimu(NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu huria
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Meatu, Simiyu, Tanzania

    Anwani ya Posta: S.L.P 44

    Simu: 028 2795 008

    Simu ya Mkononi: 0622 404 712

    Barua Pepe: ded@meatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu . Haki Zote Zimehifadhiwa.